December 11, 2018


Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Yohana Oscar Mkomola ameigomea klabu hiyo kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Namungo FC ya Lindi iliyopo ligi daraja la kwanza, imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa mshambuliaji huyo anachotaka kwa sasa ni kuvunja mkataba na klabu hiyo ili awe huru na aweze kusaka timu nyingine timu ya kujiunga nayo.

Inaelezwa katika mkataba wa Mkomola na Yanga kuna kipengele cha kuruhusiwa kuondoka muda wowote iwapo atapata timu nje ya nchi.

Kutokana na sakata hilo kati yake na Yanga, inaelezwa Mkomola tayari ameshapata timu ya kufanyiaa majaribio nje ya nchi 'Sweden' .

Inaelezwa kuwa Mkomola anaweza akasepa zake Yanga mwezi wa kwanza mwakani iwapo atatolewa kwa mkopo na endapo hatapata nafasi ya kwenda nje ndio maana anataka kuvunja mkataba na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic