Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapinzani wao Yanga inabidi watulie kwanza kuhusu viporo vyao walivyonavyo Ligi Kuu, watarejea kumaliza baada ya kucheza michezo ya kimataifa.
Manara ameyasema hayo kutokana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuhoji sababu ya viporo vya wapinzani wao licha ya kumaliza kucheza hatua ya awali na kurejea nchini bila kucheza tofauti na ilivyokuwa kwao wakati wakishiriki michuano ya kimataifa.
"Kwa sasa wapinzani wetu inabidi watulie kwanza tuna kazi kubwa ya kuweza kuiwakilisha nchi kimataifa, hili ni agizo tulilopewa na mheshimwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, serikali inatambua kazi yetu watuache kwanza tufanye kazi tukirudi tutamalizia kila kitu," alisema.
Simba wamecheza jumla ya michezo 12 kwenye ligi kuu huku Yanga wakiwa wamecheza jumla ya michezo 15 ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Akili huna, sasa hapo nani kamchana mwenzie? na kamchana nini? Kuna tofauti kati ya msemaji na mwandishi! Kajifunze japo kidogo kwa akina Bin zuiry na Edo. Unaboa sana kwa kuandika vitu visivyo na maana.
ReplyDeleteManara ni mara chache sana unaongea vitu vyenye akili. Rais kakutuma kazi gani kama si kujipendekeza jamani. Ebu acheni kulitumia hili jina vibaya.
ReplyDeleteManara anajipendekeza kwa Rais wa nchi ili apate uteuz. Sijawah kumsikia Rais akizungumzia kuhusu Simba kushiriki Klabu bingwa. Kama Rais angewatuma si angewakabidh bendera ya tz? Mpaka Rais awatume kwan Cmba ni national team? Simba wanakazi kubwa ya kumpunguza maneno ya kipuuz msemaji wao
ReplyDeleteSiku simba walipocheza na Kagera raid aliwaambia anataka kuona wanafanya vizuri hadi kuchukua ubingwa wa Afrika...sasa kama sio kuagizwa au kwa maana nyingine kutumwa ni nini? Swala LA viporo hata Yanga alikuwa navyo wiki chache zilizopita na mwaka Jana..Jana akili ya kondoo kusahau hao..Na Haji Manara alisema ungekuwa ni Simba inacheza mechi zaidi ya Tisa mfulilizo Dar? kingenuka
ReplyDelete