December 25, 2018


Kaimu Katibu wa Yanga, Omary Kaya, amesema suala lililojitokeza kuhusiana na Kamati ya Usajili kushindwa kutimiza ripoti ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, ilikuwa ni la kawaida.

Kaya amefunguka kuwa masuala kama hayo hujitokeza akieleza kulikuwa na mungiliano wa mawasiliano mpaka ikasababisha matakwa ya Kocha kushindwa kutimizwa kama alivyotaka.

Kaimu huyo amesema mazungumzo na kumalizana na Zahera yanaenda vema na akiahidi kuwa yatafikia mwafaka bila wasiwasi.

Zahera alitoa ripoti ya wachezaji kusajiliwa wakati wa dirisha dogo lakini Kamati yake iliyo chini ya Hussein Nyika ikashindwa kuikamilisha, jambo ambalo lilizua tafrani kubwa.

Katika ripiti hiyo, usajili pekee ambao ulifanyiwa kazi ni wa aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, Haruna Moshi Boban huku wengine aliowahitaji hawakusajiliwa.

4 COMMENTS:

  1. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kwanini hamsemi waziwazi kuwa tatizo ni hela na hata hela ikipatikana na kusajiliwa wachezaji wapya ingelsababisha malalamiko makubwa kwa wale wanaoitumikia timu na kutokulipwa mishahara yao kwa muda mrefu. Wangelisema hela ya kusajili wachezaji wapya zipo lakini waloostahamil muda mrefu na kuipa timu ushindi baada ya ushindi hapan

    ReplyDelete
  2. Kiukweli kama uwezo haukuwepo kulikuwa hakuna haja ya kuwaaminisha watu kuwa kamati itafanya usajili wa nguvu kama walivyokuwa wanajinasibu ilihali uwezo hautoshi,Kuwa wawazi kungetoa fursa kwa wanachama wengine kuchangia usajiri kuliko sasa hali si nzuri,hata huyo katibu nadhani alijuamapema ila aliamuakumdanganya kocha.

    ReplyDelete
  3. Acheni ujinga. Viongozi wa yanga wote mizigo. Hamna msaada kwa timu zaidi ya kutaka kushibisha matumbo yenu kupitia yanga

    ReplyDelete
  4. Yanga kuweni wepesi hata kuiga watani zenu
    ....mfano mwezi february ni kumbukumbu ya kuzaliwa klabu ya yanga iteni mechi ya kimataifa ya kirafiki na chezeni mechi ya kimataifa na klabu kongwe moja ya Afrika au Ulaya katika uwanja wa Taifa mjaze uwanja siku hiyo fanyeni umahasishaji nchi nzima na matendo ya fadhila katika jamii waalikeni mabalozi waasisi wa uhuru wa Tanganyika walio hai na wa mapinduzi ya Zanzibar ipigwe dua jangwani....halafu wachezaji watembelee hospitali na kutoa misaada, na pia uwanja wa Taifa kuwe na burudani mbalimbali halafu jioni muujaze uwanja....mtapata fedha nyingi tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic