December 25, 2018


Aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhan Kampira, amesema atanungana na wasakata kambumbu wengine waliowahi kuichezea timu hiyo kwa ajili ya kushirikiana na Kocha Mwinyi Zahera katika mambo mbalimbali.

Kampira ameeleza kuwa Yanga ya sasa inapitia wakati mgumu ikiwemo kuyumba kifedha hivyo watapambana kwa namna wawezavyo kumrahisishia kazi Zahera ikiwemo kusaka fedha za usajili.

Mkongwe huyo ambaye aliwahi kutamba na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma, ana imani mpango huo utafanikiwa na kuifanya Yanga iweze kung'ara zaidi katika mashindano ya ndani na hata nje, yaani kimataifa.

Mbali na fedha za kuikwamua Yanga na hali ngumu, Kampira pia amesema itabidi wamwombe radhi Zahera kutokana na Kamati ya Usajili Yanga iliyo chini ya Hussein Nyika, kudanganya kuhusiana na ripoti ya usajili.

Kampira amenena ni kweli uongozi haukutumiza ripoti ya wachezaji aliohitaji asajiliwe hivyo itabidi wakutane na Zahera atakaporejea ili kuzungumza naye waweze kushirikiana naye kufanya usajili vizuri.

4 COMMENTS:

  1. Nashangaa,Muda wa usajiri dirisha dogo umepita ni usajiri upi unaozungumzwa?

    ReplyDelete
  2. Hivi nauliza Ramadhan Kampira alichezea Yanga wakati wa kikosi kipi na mwaka gani

    ReplyDelete
  3. Tena uyoo nyikaa awe kipaumbelee kuomba msamaha

    ReplyDelete
  4. Yanga kuweni wepesi hata kuiga watani zenu
    ....mfano mwezi february ni kumbukumbu ya kuzaliwa klabu ya yanga iteni mechi ya kimataifa ya kirafiki na chezeni mechi ya kimataifa na klabu kongwe moja ya Afrika au Ulaya katika uwanja wa Taifa mjaze uwanja siku hiyo fanyeni umahasishaji nchi nzima na matendo ya fadhila katika jamii waalikeni mabalozi waasisi wa uhuru wa Tanganyika walio hai na wa mapinduzi ya Zanzibar ipigwe dua jangwani....halafu wachezaji watembelee hospitali na kutoa misaada, na pia uwanja wa Taifa kuwe na burudani mbalimbali halafu jioni muujaze uwanja....mtapata fedha nyingi tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic