December 2, 2018


Kipa namba moja wa klabu ya Yanga, Beno Kakolanya, amekanusha taarifa zilizoibuka takribani siku mbili zilizopita zikieleza kuwa atajiunga na wekundu wa Msimbazi, Simba, katika kipindi hiki ambapo dirisha dogo lipo wazi.

Beno ameeleza kuwa hakuna ukweli juu ya taarifa hizo na akisema bado ana mkataba na Yanga mpaka mwaka 2020.

Licha ya kukanusha taarifa za kwenda Simba, Beno hajasafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Mbeya kwa ajili ya mechi ya ligi itakayopigwa kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezaji huyo amegoma kusaifiri kutokana na kuidai Yanga stahiki zake ikiwemo fedha za mishahara ya miezi kadhaa ikielezwa pia na zile za usajili.

"Sijafanya mazungumzo yoyote na Simba, hayo yanayoandikwa hayana ukweli wowote ule. Na kuhusu kuidai Yanga ni kweli naidai, mpaka sasa sijalipwa stahiki zangu" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic