October 11, 2021


MIAKA 11 kwenye sanaa na bado anafanya vizuri sio jambo kubeza ni muhimu kumpa pongezi ili azidi kufanya kazi nzuri zaidi na zaidi, hapa namzungumzia ndegemnana, wakuitwa Lina Sanga.

Ana mengi ambayo anafikiria kuyafanya pamoja na mipango ambayo iliwahi kubuma kwa muda kutokana na sababu mbalimbali, huyu hapa anafunguka mengi zaidi kuhusu mipango yake pamoja na kazi zake:- 

"Nipo salama hilo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani kwa sasa nafikisha miaka 11 kwenye muziki kwa sasa, nilikuwa nataka kufanya miaka 10 ya Linah ila ilitokea suala la Corona na nilikuwa nataka kutambulisha EP yangu ila ilikwama hivyo mipango ikikaa sawa kila kitu kitafanyika.

Wazo la wimbo mpya Kama Yeye ilikuaje?

"Tulikuwa studio na watu wengi pamoja Ibra ambaye ameandika hii ngoma aliposkia hii biti alisema kuwa hapa kuna kitu. Tulifanya kazi kama familia na yeye aliandika.

Suala la kufanya vizuri lipoje?

"Kuna vichwa vingi tumevipoteza kwenye sanaa. Industry ya sasa imebadilika ni kama vitani tu hakuna kugeuka. Kila mtu anakwenda na upepo. Kwangu mimi naamini katika muziki mzuri.

Kuhusu kushirikiana je?

"Sapoti tunapeana na wasanii wengine na huwezi kufanya featuring na wasanii wote ingekuwa hivyo itakuwa ngumu kufanya collabo na THT wote.

"Sio rahisi na kuna changamoto zake ukisema ufuate kila kitu utachanganyikiwa mimi nafanya kitu ambacho ninaweza kukifanya na ikifika wakati nitafanya hata zile za kimataifa.

Video zako je kufanyia Bongo?

"Kila kitu ni mipango, sio nimemuona Dayna Nyange amefanya kazi na Davido basi nami leo nikasema iwe hivyo, sasa ni suala la kusubiri mbona kwenye Ole Temba iliweza kuwa vizuri.

Vipi kuhusu muonekano wako?

"Kuhusu muonekano kwa upande wa mavazi naona nipo poa na ninakwenda na wakati pamoja na mahali ambapo nipo.

Siri ya mafanikio ipo wapi?

"Uvumilivu, kujiamini na kuna muda kweli unakata tamaa ila unarudi palepale na kuanza upya, mashabiki ni watu pekee ambao wamekuwa wakinipa moyo.

Changamoto zipo ila sana kwa watoto wakike zipo nyingi.

Kuingia kwenye filamu je?

"Ni sehemu ya fursa yaani imekuwa hivyo kwa kuwa unaweza kuwa na duka unaweza kuwa na kitu fulani hivyo ni sehemu tu ya fursa.

Ngoma mpya je?

"Kuna ngoma yangu mpya ya Singeli ambayo inakuja inazungumzia Mke mwenza lakini sio kama ile ya Zuchu.

Mauzo ya mtandaoni yapoje?

"Bado Watanzania tupo nyuma kwenye masuala ya mitandao, unaweza kuachia kazi watu wanahitaji uwatumie, bado Watanzania tupo nyuma, nimetoa Ole Temba lakini bado sijajua kwa sasa imefikisha view ngapi.

Kwa upande wa tuzo je ipoje?

"Tuzo za Afrima ni wewe mwenyewe unafanya application ni kile ambacho ninakijua kwa kuwa niliwahi kufanya Application na nilikwenda mpaka Lagos pia. 

Kuna watu unawatazama kwenye kazi?

"Tunaangalia Malegendari wakubwa namna wanavyofanya hao akina Beyonce wanavyofanya, muziki unakwenda na fasheni na ninavaa nguo kulingana na sehemu ambayo ninakwenda.

Ishu ya malezi je?

"Upande wa malezi sio kitu rahisi ila mimi ninamuachia Mungu kwa sababu ninaamini kwamba mimi kuna vitu sifanyi ambavyo wazazi walikuwa wanafanya. 

"Ninachomuombea mwanagu afanye vitu sahihi. Kwa sababu mimi tayari nimeshakuwa hapa basi kila kitu kinakuwa tatizo. Ila kuna watu ambao wapo nyuma wanafanya mabomu makubwa kuliko yangu.

Umeshawahi kujuta kuwa maarufu?

"Kuna wakati huwa naujutia lakini kwa kuwa imetokea basi ipo hivyo.

Tattoo zako je?

"Kuna moja imeandikwa Talent kwa lugha ya kichina ambayo ipo, love ni ile inayohusu upendo kwa muziki ni kitu ambacho ninakipenda na pia kuna ala ya muziki ambayo ninaifanya.

Mipango ipoje kwa sasa?

"Vitu vingine ikifika itafahamika. Na kuna vitu ambavyo nafanya nje ya muziki ila bado sijaruhusiwa kufanya.


Kuhusu album je?

"Nina mpango wa kutoa albamu mwakani kwa sasa acha wengine wafanye, nilikwama kwenda kwenye albamu ya Kiba kwa kuwa sikuwa Dar na niliweza kumwambia kwamba ametisha.

Ndoa je?

"Ni majaliwa ya Mungu na bado sijajua kwamba kwa sasa baba atataja mahali bei gani, kiutamaduni sisi huwa hatutaji mahali ni mzee ambaye anapanga.

Unahitaji kuacha alama gani kwenye muziki?

"Ikitokea nimeacha muziki nadhani kuna kitu kitakosekana hasa kumpata Linah kama ilivyo kwa sasa huwa namkumbuka sana Vanesa nadhani kuna kitu ambacho kinahitaji kujaziliwa na Vanessa mwenyewe.

Wewe na Babalevo je?

"Niliwahi kuonana na Babalevo studio za Kama Kawa ila niliogopa na nilikuwa naona woga kwa sababu mimi nilikuwa ninaimba gospel.

Diamond ama Harmonize?

"Mimi sina timu kwa kuwa kote nafanya mawasiliano nao kwa kila mmoja, Diamond nafanya naye kazi hata Harmonize pia nafanya naye kazi sina tatizo nao," anamalizia ndegemnana.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic