Mlezi wa Serengeti Boys, Dkt Reginald Mengi mapema leo aliandaa hafla fupi kwa ajili ya kukipongeza kikosi cha Srengeti Boys kilichotwaa ubingwa wa kombe la Cosafa, hivi karibuni nchini Botswana.
Katika hafla hiyo Dkt Mengi aliwapongeza kwa ubingwa huo huku akiitoa zawadi ya fedha kwa wachezaji na benchi zima la ufundi huku akiwaambia kuwa kutwaa kombe hilo ni moja ya safari nzuri ya kuelekea kutwaa ubingwa katika michuano ya Afcon inayotarajiwa kurindima mwakani hapa nchini.
“Hii ni historia kwa timu yetu hii ya vijana kufanya vizuri kwenye Mashindano mawili ikiwemo kombe la Cosafa, hivyo wanastahili pongezi.
“Pia niipongeze serikali kwa sapoti kubwa wanayoendelea kuitoa katika timu yangu hii ya vijana, hivyo tutampatia kombe hili mheshimiwa Rais Magufuli kama zawadi ya krismasi, kwani tunajua atafurahia kwakuwa ni mmoja ya viongozi wapenda mafanikio.
“Mbali na zawadi hizi nilizotoa hapa naomba niwaambie tu vijana wangu wa Serengeti Boys kuwa zawadi hii ya leo nimelazimika kuipinguza baada ya kushauriwa kuwa umri wenu bado ni mdogo sana hivyo kwakuwa mimi nitaendelea kuwa nanyi, nitatatumia mali zangu zote ili nihakikishe huko badaye maisha yenu yanakuwa mazuri,” alisema Mengi.
0 COMMENTS:
Post a Comment