December 11, 2018



Kikosi cha Halmashauri ya Kinondoni, KMC kimeanza maandalizi dhidi ya mchezo na Tanzania Prisons utakaochezwa Jumamosi katika uwanja wa Uhuru.

KMC iliyo chini ya kocha Ettiene Ndayiragije mchezo wao wa jana nyumbani walikubali sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC na kuwafanya wagawane pointi moja.

Ofisa habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa wamejifunza kupitia makosa hivyo benchi la ufundi litafanyia kazi kuhakikisha wanapata matokeo.

"Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila mmoja anataka matokeo, benchi la ufundi limeyaona makosa na litayafanyia kazi kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons," alisema.

KMC imecheza michezo 15 ikiwa na pointi 18 inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic