Mjumbe wa Baraza la wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ameshangazwa na baadhi ya viongozi wa matawi wa ya klabu hiyo baada ya kusema kuwa amemtumkana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Kapteni mstaafu George Mkuchika.
Hatua hiyo imekuja kutokana na viongozi hao kukutana juzi katika mkutano wa matawi ambao ulimwelezea Akilimali kuwa amemtukana hadharani Mkuchika ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini ndani ya klabu.
Akilimali ameibuka na kueleza kuwa huo ni uchonganishi kwake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, jambo ambalo akilikanusha vikali.
Mjumbe huyo amefunguka kukanusha kumtukana Mkuchika na badala yake ameeleza kuwa alisema ameshindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya Yanga.
Ameeleza kukosoa mapungufu ya Mkuchika pekee juu ya nafasi yake ndani ya klabu kulingana na wadhifa aliopewa na si kumtakia matusi kama ambavyo baadhi ya viongozi walivyoeleza.
Akilimali amesema anaamini kuna watu wanatumika kujaribu kumsemea kwa serikali ili imchukulie hatua za kisheria lakini akiwatumia salaam kuwa wajaribu kutathimi kauli zao kabla hayajawatokea puani.
Mwisho Akilimali amezidi kusisitiza ni vema uchaguzi Yanga ukafanyika kama kawaida ili kupata viongozi wengine kutokana na klabu hiyo kuwa na mapungufu mengi mpaka sasa ya viongozi ambao wanapaswa kuwa madarakani.
0 COMMENTS:
Post a Comment