December 3, 2018


Kikosi cha Yanga ambacho mpaka sasa katika michezo 13 hakijapoteza mchezo hata mmoja na leo kitashuka kumenyana na Prisons kimepewa mzigo wa kushinda na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera.


Mchezo huu unakuwa ni watatu kwa Yanga kucheza nje ya Dar es Salaam, wana kumbukumbu ya kushinda mechi 2 walizocheza nje ya  Dar kwa kuchukua pointi sita katika michezo ya kanda ya ziwa.

Nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa wamejipanga kuweza kulinda rekodi ya timu ambayo wameanza nayo na kocha amewapa kazi.

"Kocha amemaliza kazi yake kwa kutupa mbinu ambazo tutazitumia ili kupata matokeo mbele ya wapinzani wetu Prisons tunaamini tutapata matokeo.


"Kazi kubwa imebaki mikononi mwetu kwa kuwa upande wa mwalimu ameshamaliza, morali ya wachezaji ni kubwa kwa kuwa tunajua mashabiki na uongozi unahitaji nini," alisema. 


Yanga wamecheza michezo 13 na kufanikiwa kushinda michezo 11 na kutoa sare 2 wakiwa na pointi 35 ni vinara wa ligi huku wapinzani wao Simba wakiwa nafasi ya 3 na kuachwa kwa pointi 8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic