December 3, 2018


Mshambuliaji wa Simba raia wa Rwanda, Meddie Kagere amesema kuwa wamekwenda Eswatini kutafuta ushindi katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.


Simba wametua jana nchini Eswatini, watacheza kesho huku wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 waliyopata katika uwanja wa Taifa.


Kagere amesema wanatambua mashabiki wanahitaji ushindi hivyo watapambana kuhakikisha wanapata matokeo ugenini.

"Tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo tukiwa ugenini hivyo kama wao waliweza kupata bao 1 nyumbani nasi pia tunaweza kwenda kushinda kwao inawezekana.


"Ushindani ni mkubwa ila tunacheza tukiwa ni timu wakati wa kutafuta matokeo ili kuweza kusonga mbele, mashabiki waendelee kutupa sapoti tuna imani ya kufanya vizuri," alisema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic