Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo hivi karibuni anatarajia kupokea kiatu kipya cha kuchezea kutoka nchini Uturuki baada ya kununuliwa na mmoja wa wafuatilia wa soka nchini Tanzania, Mzee Karama.
Mdau huyo mwenye duka la michezo la Just Fit lililopo Mlimani City jijini Dar amemnunulia kiatu hicho mshambuliaji huyo sambamba na beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambavyo atawapa hivi karibuni kwa ajili ya kuvitumia kwenye michezo ya ligi.
Mzee Karama ameliambia Championi Ijumaa, kuwa anamletea Makambo viatu hivyo kwa ajili ya kuongeza idadi ya mabao ambapo tayari ameshavilipia.
“Nipo Uturuki na nimenunua viatu vya Makambo na Ninja ambavyo nawaletea, tayari nimeshavilipia. Namletea Mkambo hili mabao yaongezeke,” alisema Mzee Karama.
CHANZO: CHAMPIONI
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Asante
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Wadau na washabiki kama hawa wanatakiwa sana katika soka la Tanzania. Binafsi, nimpopngeze Mzee Karama.
ReplyDeleteViatu!ndio unatuandikia.. Akipata na soksi za ujerumani tuambie basi
ReplyDeleteKwan Makamba anacheza peke yake uwanjani kuiwakilisha Yanga? Mnunulie na Ajibu, Tambwe, Paul Godfrey, Gadiel, Kabwili, wote hao wazuri, kusema kweli tuache kubagua wachezaji. Ukitaka haki, nunua seti nzima ya viatu kwa wachezaji wote, maana hata hao walio reserve Sipo siku yao watacheza.
ReplyDelete