December 21, 2018


Baada ya kuwatumia wachezaji ambao amekuwa hawatumii mara kwa mara, Kocha wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuwa wanapambana kwa nguvu na kuonyesha kiwango kizuri.

Katika mchezo wa juzi dhidi ya KMC ambao walishinda kwa mabao 2-1, Adam Salamba na Said Ndemla walifunga mabao na kuipa ushindi timu hiyo katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa.

Kocha huyo alisema alifurahishwa na kiwango ambacho walikionyesha licha ya kuwa wengi wao ilikuwa mara yao ya kwanza kucheza katika ligi kuu msimu huu.

“Nimeridhika na ushindi wa pointi tatu na timu yangu mpya ile ambayo ilicheza jana na hiyo imedhihirisha kuwa wachezaji wangu wote wana uwezo wa kupambana bila tatizo.

“Lakini sasa tunaangalia mechi iliyopo mbele yetu dhidi ya Nkana kuona ni jinsi ngani tunaenda kupambana, zaidi niendelee kuwashukuru mashabiki wa Simba ambao wamekuwa pamoja nasi katika michezo kwa kuja kutusapoti,” alisema Mbelgiji huyo.

Baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawana uhakika wa kikosi cha kwanza lakini walicheza juzi ni Said Ndemla, Deogratius Munishi ‘Dida’, Rashid Juma, Zana Coulibaly na Mzamiru Yassin.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

2 COMMENTS:

  1. Acha ujinga wa kupotosha watu wachezaji ambao hawana uhakika kwenye kikosi cha kwanza unamtaja coulibaly na wakati ndo kwanza kasajiliwa huo ni ujinga unaoufanya

    ReplyDelete
  2. Acha ujinga wa kupotosha watu wachezaji ambao hawana uhakika kwenye kikosi cha kwanza unamtaja coulibaly na wakati ndo kwanza kasajiliwa huo ni ujinga unaoufanya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic