December 14, 2018






NA SALEH ALLY
MOJA ya matamanio makubwa nimekuwa nayo siku nyingi sana ni kuona Tanzania inakuwa na wachezaji wengi wa kulipwa nje ya nchi yetu.

Wachezaji wa kulipwa ndiyo dawa ya hesabu za muda mfupi kujiondoa tulipo. Baada ya hapo tunaweza kuanza kupiga hesabu za muda mrefu ambazo ni suala la vijana ambalo linahitaji subira kubwa.

Kama tukiwa na wachezaji wengi wa kulipwa, maana yake ni hivi, watakuwa ni tofauti na waliojifunza mengi, rahisi kwao kutoa msaada kwa Tanzania ili tuweze kupiga hatua kwa kuwa watajifunza mambo mengi wanapokuwa nje ya Tanzania.

Wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania wanakutana na mengi ambayo hawakuwahi kujifunza na baada ya hapo, wanaanza kujua kile ambacho awali hawakukijua. Mfano angalia wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania wanavyojua kuhusiana na umuhimu wa timu ya taifa kuliko walio hapa nyumbani.

Wengi walio hapa nyumbani wanaweza kuona timu ya taifa ni kuchoshana na haina maana. Lakini kama unacheza nje ya Tanzania, timu ya taifa ni sehemu ya thamani yako na heshima unayoweza kupewa huko uliko, hivyo wengi wanaocheza nje wanaichukulia kwa juu sana.

Kidogo nimeanza na mzunguko lakini nataka kulenga kuhusiana na Shaban Iddi Chilunda. Kinda Mtanzania anayecheza katika kikosi cha Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania akiwa na Klabu ya Tenerife.

Hivi karibuni, Tenerife imetoa siku kadhaa hadi mwisho wa mwezi huu wa Desemba, kama Chilunda atakuwa ameshindwa kujirekebisha katika suala la kiwango chake, basi ataonyeshwa mlango wa kutokea.

Inaonekana amecheza dakika 22 tu katika mechi za mashindano tangu amejiunga na timu hiyo. Wao wanaona si sahihi na msisitizo ni kwamba, wakimpa nafasi haonyeshi juhudi.

Nashukuru nina nafasi ya kupata taarifa kuhusiana na hilo na nilijaribu kudadavua kwa lengo la kujifunza na kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na huyu kijana wetu kutoka Tanzania.

Natambua mafanikio ya Chilunda ni hatua kwa mpira wa Tanzania na ningetamani kumuona anategemewa na Tenerife na baadaye aende sehemu nyingine kubwa zaidi ikiwezekana La Liga na kadhalika.
Kote nilikofuatilia wameniambia kitu kinachofanana na ninaamini hawawezi kuwa na sababu ya kumbania Chilunda hasa kama atakuwa msaada katika kikosi chao, maana yake hawawezi kumlalamikia.

Kama wanasema hajitumi na haonyeshi juhudi, basi lazima kutakuwa na tatizo. Lazima ayafanyie kazi matatizo yake badala ya kulalamika.

Nimeelezwa kwamba naye alisema timu haimpi nafasi, lakini timu inasema ikimpa nafasi haonyeshi chochote na wanaona kama kumpa nafasi wanaipoteza ndiyo maana wameamua kutoa masharti.

Kama utakwenda kucheza Ulaya halafu ukataka kuilazimisha timu ifanye unavyotaka, hakuna ubishi lazima utafeli. Hili limewatokea wachezaji wengi waliotokea Afrika na Tanzania ikiwemo.

Sasa kwa Chilunda anaweza kuona kuondoka Ulaya ni sawa kwa kuwa Tanzania anahitajika. Lakini hili ni kosa kwa kuwa kwa uwezo wake na alipofikia anatakiwa kuondoka Tanzania na kuendelea kupambana.
Pia ishu hii ya Chilunda inatuonyesha kucheza Ulaya ni zaidi ya uwezo wa uwanjani pekee. Suala la kujituma, nidhamu ya usikivu na matendo ni mambo ambayo hapa nyumbani yapo kwa kiwango cha chini.

Sasa mchezaji anapokuwa timu kubwa kama Simba, Yanga au Azam FC, anaona kama ameyaweza yote na anapopata nafasi nje anaonekana yuko katika kiwango cha chini na yeye anashindwa kukubaliana na hilo. Chilunda anapaswa kujitazama mara mbili na ikiwezekana apambane kupata nafasi ili maisha yawe magumu mwanzo na baadaye asonge mbele.

Kumbukeni, Mbwana Samatta awakati anatua TP Mazembe alimkuta nahodha Tresor Mputu ndiye kila kitu. Lakini mwisho alifanikiwa kuwa mfalme, haikuwa rahisi. Hivyo kama mnatamani kuwa kama Samatta, mjue hakufika hapo kwa ndoto za kulala usingizi wa pono, alipambana.

6 COMMENTS:

  1. Kwanini unakwenda mbali kumzungumza chilunda vipi Mohamed Rashid aliechemsha pale Simba, vipi kaheza au Mbaraka Yusufu? Nimeanza na wachazaji hao wachache vijana kwakuwa tuliona tayari walishaiva hata kucheza Ulaya na wakati wanasajiliwa Vilabu vya hapa nyumbani watu wengine walilaumu kwanini hawakutafuta timu nje ya nchi? Sina hakika lakini kwa hulka za kitanzania naamini mchezaji akitoka Namungo FC akienda nje kubahatisha anaweza kutoka kuliko akitoka Azam FC kwa watanzania au wachezaji wa kitanzania wakipata raha kidogo ya maisha huwa wanabweteka baada ya kuongeza bidii. Inawezekana chilunda anaiwaza na ana imiss sana Azam au hana mtu wa karibu wa kumshauri kikazi. Na ndio maana tuliokuwa tukipigania idadi ya wachezaji kumi 10 wakigeni ni lazima kwa sababu vijana wetu wanahitaji kushinda ushindani wa hapa nyumbani kwanza ikiwezekana ushindani wa Africa kwanza kabla kufikiria kwenda ulaya. Mfano kama Mohamedi Rashid au Marcel Kaheza wangemudu kuwachomesha mahindi akina Kagere pale Simba pasi sidhani kama wangelipata nafasi ya kucheza nje ya nchi halafu washindwe. Hata hiyo Azam ya chilunda na ya sasa tofauti akirudi anaweza kuishia benchi.kama ilivyokuwa hapa tanzania kudai kuwa mchezaji wa kigeni awe na kitu cha ziada ili awaridhishe wenyeji na nchi za Ulaya vile vile. Wakikuona upo wa kawaida kawaida tu huoneshi makeke halisi ya mtu mweusi katika kujituma upo laini laini tu basi watakutema tu kwani na wao wanavijana wao wengi tu wa kawaida wanaweza kufundishika kirahisi na wakafanya vizuri bali wanachotafuta kutoka kwa wachezaji wetu ni mchezaji mwenye uwezo wa ziada mwisho wa habari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea ukweli mtupu kamanda, wachezaji bado sana inabidi turuhusu wachezaji wengi wa kigeni, Leo tunasema ngassa,kagere,okwi ni wazee je kuna vijana wangapi wa kumuweka okwi au kagere au ngassa benchi?,Yondani mzee lakn ndo tegemeo la ulinzi utamuacha vipi benchi, ndomaana nikiangalia hata suala la boban kusajiliwa yanga naona sawa tu, kuna kijana gani wa kumsubirisha kwenye mbao haruna moshi?, Tatizo ni kujituma, nidhamu na malengo ndo wachezaji wetu wanachokosa

      Delete
  2. Tatizo la Chilunda ni aina ya striker anaesubili kulishwa ambapo mpira was Sasa tayr umebadilika. Lazima afanye Kaz ya ziada kama anataka kucheza ulaya.

    ReplyDelete
  3. Kwanza Huyo chilunda ni mbinafsi anapenda sifa

    ReplyDelete
  4. Next season wachezaji wa kigeni waongezwe wafikie hata idadi 12.hawa wachezaji wazawa wanawaza kucheza ndondo cup viwanja vya Tandika.Mpira ni biashara hivyo inahitajika ushindani na kumbuka klabu zinahitaji kudhaminiwa na wengine wana bet.Tuache masihara la sivyo tutaendelea kuangalia ligi za Ulaya kwenye luninga

    ReplyDelete
  5. Nimewahi kushuhudia mazoezi ya Simba pale Gymkhana club na kubaki mdomo wazi kuona majority ya wachezaji wazawa hawajitumi na kufanya mizaha utafikiri ni ameature players.Kwa kweli wachezaji wengi hawajitambui kuwa mpira ni ajira ina
    yokupa mshahara kwa ajili ya maisha yako na Familia.Majuzi tumesikia Kagere na Okwi walipata ofa ya kununuliwa na klabu zingine za Africa lkn sijasikia ofa kwa mzawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic