December 29, 2018


KOCHA wa Lipuli FC, Seleman Matola amesema kuwa jeuri ya kikosi chake kuwa na mwendelezo wa kupata matokeo mazuri ni  sare waliyoipata na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu waliocheza uwanja wa Taifa.

Baada ya sare hiyo, Lipuli walifanikiwa kukusanya pointi 9 katika michezo ya Ligi kuu waliyocheza ambayo ni pamoja na Mbeya City kwa kuwachapa bao 2-0 wakiwa  ugenini, walishinda pia dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Samora, Biashara United Samora  na kesho watakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda SC.

Matola amesema kuwa vijana walipata kutambua uwezo walionao hasa baada ya kutoa sare na kikosi ambacho ni cha gharama kubwa tofauti na wao hali iliyowajenga kisaikolojia.

"Kwa sasa Lipuli tupo vizuri baada ya kupata sare na Simba kuna nguvu mpya ambayo imeingia kwa wachezaji kwa sasa wanajiamini na kutumia uwezo wao wote wakiwa uwanjani hali inayosaidia kuweza kupata matokeo hivyo bado moto hauzimwi kwa sasa.

"Tumejipanga kufanya vizuri katika michezo yetu yote tutakayocheza kwa sasa hilo linawezekana kwani mpira ni mchezo ambao hauwezi kuficha matokeo yake yanapatikana uwanjani, mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema Matola.

Lipuli wamecheza michezo 17 wakiwa wamejikusanyia pointi 22 baada ya kushinda michezo 5 wakipata sare michezo 7 na kupoteza michezo 5 leo watakuwa uwanjani Samora kucheza na Ndanda SC ambayo inashika nafasi ya 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic