MCHAKATO wa usajili wa filamu katika msimu wa pili wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Sinema Zetu 'SZIFF' umekamilika kwa kukusanya filamu 235.
SZIFF imekamilisha mchakato kabla ya kuanza hatua ya upigiaji kura wa filamu hizo kwa ajili ya usiku wa tuzo za SZIFF unaotarajia kufanyika Februali 23, mwakani katika ukumbi wa Mlimani City Dar ambapo washindi 24 watangazwa na kupatiwa tuzo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, mapema leo, mratibu wa tamasha hilo Sophia Mgaza alisema kuwa mchakato huo umekamilika baada ya kufunguliwa Oktoba mwaka huu kabla ya kufungwa Novemba 30.
Sophia alisema kuwa tamasha la mwaka 2019 litapitia hatua tatu muhimu ambayo ya kwanza itakua ni kuonyeshwa filamu zote zilizosajiliwa kwa muda wa mwezi moja wakati jopo la majaji litakapokuwa lifanya kazi yake.
Mbali ya Sophia, Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwigelo ambaye ni mlezi wa tuzo hizo, amewapongeza Azam TV, kupitia channeli ya Sinema Zetu kuwa wameongeza fursa ya wasanii wa ndani kuweza kushindanisha kazi zao tofauti na miaka iliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment