December 25, 2018


Timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Wilayani Rufiji, Kiluvya United imenunuliwa na Kampuni ya Mchengelwa Foundation iliyo chini ya Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengelwa.

Mchengelwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amefikia maamuzi hayo kwa ajili ya kuifanya Rufiji iweze kufika mbali kisoka.

Mchengelwa Foundation imeamua kuibatiza jina jipya Kiluvya ambayo sasa itakuwa inajulikana kwa jina la Rufiji United kutoka Kiluvya.

Tayari Rufiji United itakuwa chini ya udhamini wa kampuni hiyo huku mipango ya kusaka wadhamini wengine ikiendelea hivi sasa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic