December 16, 2018


Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Mwalimu Alex Kashasha, amesema Simba wanapaswa kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia.

Kashasha ameleza kuwa katika mchezo wa jana Nkana walionesha uhai mkubwa na kuwapa wakati mgumu Simba haswa kwenye safu ya kiungo chao jambo lililowafanya wajiamini kuutandaza mpira vizuri.

Kashasha amefunguka kuwa Nkana waliingia uwanjani kushindana na wakiwa na mbinu za kuisoma Simba mapema na ndiyo maana waliweza kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa.

Katika mchezo huo ambao Nkana walishinda kwa mabao 2-1, Kashasha amewataka Simba kuhakikisha wanajipanga vema kutumia faida ya uwanja wa nyumbani ambapo watapaswa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 pekee ili wasonge mbele.

Simba watakutana na Nkana kwenye mchezo wa marudiano Disemba 23 2018 jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa.


8 COMMENTS:

  1. sasa mbinu gani kawapa. umesoma wapi?

    ReplyDelete
  2. Nionavyo Mimi:- Simba inapaswa kurekebisha haya:- (1) Mechi ya marudiano jamaa watajipanga upya japo watoe sare, (Huenda wakajilinda kwa nguvu sana kwa kujaza mabeki wengi na kushambulia kwa kushtukuza na kwa kasi kwa kuwatumia viungo wao wenye kasi. Hapa forward wawe organized na wawe na ushirikiani wa haraka wa kuongeza idadi ya watu ktk ushamvuliaji inapobidi na si kumuacha 1 dhidi ya beki 3 au 2 dhidi ya 4.Hapa viungo wawe sharp kusaidia kushambulia na kukaba kwa pamoja, aidha fowadi wawe aggressive wanapokuwa eneo LA hatari wajaribu Ku force inapobidi hii italazimisha defenders kucheza faul kitu kinachoweza kupelekea penart au mipira ya adhabu. (2) Mipira ya pembeni;- hapa ndipo napoona gap LA Kapombe na Asante Kwasi, Mohammed Hussein anatakiwa afanye mazoezi ya kutosha ktk kupiga krosi zenye macho, ni mzuri na mwepesi wa kukaba kushambulia Ila cross Mara nyingi hazina macho (ajirekebishe) tofauti na Kwasi yy ana uwezo was kutoa cross murua na hata kufunga kabisa japo kidogo yupo slow. Kwa kuwa jamaa watacheza solid defence ktk mechi ya marudiano kwa kujaza beki wengi has a watakapokua na matokeo yanayowabeba (kwa muno wangu) mipira ya cross (zenye macho) iwe ya kutosha ili kuwalisha forward, na hata fowadi na wenyewe wajiongeze ktk kuji position ili kutendea haki nafasi za mipira hii, na ni vema waende pamoja kw a timing na mawasiliano mazuri sana ili kuwapoteza mabeki - Hapa ndipo najiuliza zile diving header za Kagere (Ktk mechi za kwanza za ligi) na hata Bocco (Baadha ya mechi km ile ya kirafiki na AFC Leopards) wazifanyie mazoezi tena japo kwa kiasi huenda wakatubeba kw a kufunga mipira ya namna hii. Upande was kulia - cross huku ndipo majanga. Gyan aongeze kasi ktk kuwatoka mabeki na kutoa cross (zenye macho). Huwa najiuliza hivi ni kwa nn Simba haipendi kusajili/kuwatumia ma wings wenye kasi? Kuna dogo aliekua team B Rashid Juma ni mzuri (japo uzoefu bado), coach anapaswa kumuandaa na kumkomaza ktk mechi za ligi hata kwa kupata nusu SAA ya kucheza hata ktk kila mechi hasa mechi nyepesi. Hapa ikiwa tungekuwa na wing aina yake ambae ni mzoefu hakika angetubeba mechi km hizi na has a iliyopita. (3) Beki:- NKANA wana kasi sana karibu wachezaji wote has a viungo na fowadi. Hapa inatakiwa kutumia akili sana kuwadhibiti, jamaa kule kwao hawakuridhika na matokeo Yale, hivyo watajipanga na kuja tena kwa kucheza kwa nguvu zaidi, Nionavyo ni kuwa wametuzidi kasi (kwa kuwalinganisha na Simba) hivyo hapa alipaswa awepo beki aina ya Juuko, kwa namna achezavyo (km akiamua kujituma km achezavyo timu ya taifa UGANDA) Juuko sidhani km tungefungwa lile goli LA 2. Tatizo lake nae nidham hamna, ni bora angelitimuliwa mapema ili atafutwe mbadala wake. Hapa pia inapaswa timu ikipoteza mpira wakabe kwa umoja na ushirikuano mkubwa, kila mmoja awe na jukumu LA kuzuia/kutafuta mipira ili kuzuia move zao zenye kasi inayobebwa na wachezaji wao wenye kasi, style hii ya kukaba kw pamoja baada ya kupoteza mipira (km wanavyocheza Barcelona wanapopoteza umiliki was mpira) itawamudu kuwazuia Nkana. (4) Matumizi mazuri ya mipira iliyokufa;- Timu iwe na uchungu wa kupoteza kila nafasi ktk free kicks na kina inazopata, mbinu za kufunga kwa kutumia mipira iliyokufa ziboreshwe ili walau ktk 3 basi walau goli 1 lipatikane. Aidha ni vzr fowadi wawe wana move mda ote kabla ya mipira kupigwa kuliko kusimama km mlingoti jambo ambalo linapelekea kudhibitiwa kirahisi. Nionavyo mm pindi mpira uliokufa utokao pembeni kama cross wanapaswa wachezaji wa move kwenye lango LA adui hata 3 au 4 (fowadi 2 na viungo/mabeki 2). (5) Kupoteza umakini wa kujilinda wakati wa mashambulizi mfululizo:- Timu imekua na kasumba hiyo, sasa hapa Barcelona style ya ukabaji pindi wanapopoteza umiliki itumike sana

    ReplyDelete
  3. (6) Double cross/Triple cros na V-pass:- wings au mabeki wanaosaidia kushambulia kupitia pembeni wawe wanatoa pasi ndefu (badala ya kutoa cross) kwa wing upande wa 2 ambae nae anatoa cross kwenye eneo LA adui na hapo fowadi wawe wameshajipanga kwa kufunga ktk lango, Hii Itawachanganya defenders wao na kufungika kirahisi. (7) Kucheza jihadi na tahadhari ya kadi za njano na nyekundu;- wachezaji wajitume na wawe umakini ili kuepuka kadi za mapema. (8)Kujiandaa na penati;- lolote laweza kutokea, ikitokea matokeo yamekua 2 - 1. Hadi I mwisho wa mchezo, Ni vema timu itenge muda wa mazoezi ya penati. Kingine Manula ajiongeze kufanya mazoezi ya kudaka mashuti ya mbali, ni kipa mzuri sana tatizo lake ni hapo. Nadhani 80% ya magoli aliyofungwa ni ya aina hii.

    ReplyDelete
  4. Nkana FC wazuri lakini si wazuri wa hivyo kwa Simba. Uzuri wa Nkana ulitokana na kutumia vizuri mbinu za nje ya uwanja zaidi kuisoma Simba na walipoingia uwanjani walijua kabisa wapi pa kuipiga Simba. Inaonekana Nkana walikuwa wajanja zaidi kupata taarifa za Simba na game plan yao kuliko Simba walivyokuwa na taarifa za Nkana. Ilikuwa vigumu kupata kuangalia mechi zilizopita za Nkana mitandaoni na nadhani mpaka hivi sasa lakini ni rahisi sana kuzipatia taarifa za Simba na mikakati yao hata kuangalia kwa nafasi ya kutosha mechi zao hivi karibuni. Hapana shaka Nakana waliwasoma Simba zaidi au kupewa taarifa yakwamba ukiishika Simba kwenye kiungo basi huwa wamekwisha. Kazi kubwa ya kufanya kwa Simba kuelekea mechi ya marudiano ni kupitia marudio ya video ya mechi ya kwanza ili kupata muda wa kuwasoma zaidi Nkana. Vile vile Simba wanatakiwa kupata marudio ya video ya mechi mbili za Nkana kati yake na Songo ya Msumbiji hasa mechi yake aliyocheza ugenini kule msumbiji ili kupata kujua Nakana anachezaje anapokuwa ugenini. Simba wanatakiwa kufanya hivyo kwa haraka. Nkana ana uzoefu wa mashindano ya Africa na mbinu zote za nje ya uwanja kuliko Simba ili kumuondoa Nkana nje ya mashindano haya basi lazima kazi kubwa ifanyike kuanzia uongozi mpaka,mashabiki na wachezaji pia. Nkana ni moja wa vigogo na kipimo kizuri kwa Simba kujirizisha ubora wao wa ndani na nje ya uwanja kabla ya kuingia hatua ya makundi. Kila mtu anatamani kuwa kocha lakini kama ningekuwa kocha wa Simba basi ningemsogeza Chama mbele zaidi na nafasi yake ikajazwa na khassan Dilunga. Itategemea na ufiti wa wachezaji wenyewe lakini wachezaji kama kwasi, Juuko, Kotei ni wa kuandaliwa ili kuja kuongeza nguvu kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mechi iliyopita. Lakini kama kocha atashikilia na msimamo wake wa kuchezesha kikosi kile kile cha mbabane swallows basi Simba wataabika tena pengine kuaga mashindano,mkazo uekwe hasa kwenye safu ya ulinzi

    ReplyDelete
  5. simba wanafungwa magoli yaleyale wachezaji wanaachiwa free kupiga mashuti wawa badala ya kumkabili fowadi anarudi nyuma ni muhimu Juuko acheze ikiwekana Nyoni apande kiungo ili kuongeza uimara wa beki ya simba, Boko ni mzigo kwa timu Mo Ibrahim sijui kwanini hawampi nafasi, Mohamed Huseni awe anapiga cross za maana badala ya kupooza mashambuli pia wakina mkude wawe makini kwenye kukaba Simba sijui kwanini baada ya mechi na wasazi hawakwenda kuisoma Nkana

    ReplyDelete
  6. juuko murshihid ni mhm saaaaana pamoja na matatizo yake akicheza mechi ijayo ushindi 100% ni beki aliyeweza kuwazuia washambuliaji wote hatari wa kimataifa akiwa uganda NA simba waulize almasry na timu nyingine japo ana kiburi ila kwa kipindi hiki saikolojia itumike ili arudi mchezoni na tuendelee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic