NGOMA NGUMU, WANACHAMA YANGA WAGOMA KUFANYA UCHAGUZI
Matawi ya Yanga, Kanda ya Kinondoni yameafikiana kwa pamoja kutoshiriki uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo mwezi ujao, Mwenyekiti wao, Shabani Msonja amethibitisha.
“Hatupo tayari kwa uchaguzi ambao TFF watausimamia na kama watatuhitaji sisi Kanda ya Kinondoni, sio peke yetu bali hata kanda nyingine pia hawapo tayari kwa ajili ya uchaguzi,’’alisema mbele ya wanachama wengine kwenye mkutano wao, Magomeni Mwembechai, Jijini Dar es Salaam.
“Ndugu zetu Jonas Tiboroha na Mbaraka Igangula wamejitakia matatizo wenyewe maana wanagombea kuiongoza timu kwa mwaka mmoja. We fikiria Yanga na matatizo yetu mwaka mmoja unatosha kufanya maendeleo gani.
Sasa wajiandae kuja na polisi kila watakapotaka kuingia ndani ya jengo la Yanga,”alisema kiongozi huyo. Msonja ambaye alisema msimamo huo ni wa matawi 45 ya Yanga kwenye Kanda hiyo inayojumuisha na Ubungo.
Yanga inapaswa kufanya uchaguzi wake Januari 13 2019 kwa mujibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ikishirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
CHANZO: CHAMPIONI
Sasa ayya matawi kazi yao uchaguzi tu masuala mengine ya Club awausiki
ReplyDelete