Xherdan Shaqiri amesema hapendi kukaa bench lakini mpira unampa nafasi mchezaji bila kujali muda gani.
Shaqiri aliingia kipindi cha pili na kufunga mabao mawili yaliyoiwezesha Liverpool kuitwanga Manchester United kwa mabao 3-1.
Wakati anaingia matokeo yalikuwa safe ya 1-1 lakini mashuti yake mawili yaliyowagonga mabeki wa manchester na kumpoteza kipa David De Gea, yaliipa Liverpool ushindi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa Anfield.
“Siwezi kufurahia kukaa benchi, lakini mpira ndivyo ulivyo. Unakupa nafasi kila wakati na inawezekana ukawa msaada zaidi ukiwa unatokea benchi.
“Ningeweza kuanza na nisingefunga. Hivyo jambo sahihi ni kuitumia nafasi unayoipata bila kujali ni wakati upi,” alisema.
Mshambuliaji huyo raia wa Uswiss aliwahi kung'ara na FC Basel ya nchini mwao lakini Bayern Munich ya Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment