December 22, 2018


Hatma ya Kipa, Beno Kakolanya wa Yanga kuendelea kuitumikia klabu hiyo ipo mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera baada ya kumkataa, ambapo kwa sasa wanasubiria uongozi wa klabu hiyo kuweza kuzungumza na kocha huyo ili kujua lini atarejea.

Kakolanya kwa sasa yupo njia panda kuweza kurejea katika kikosi hicho mara baada ya kumalizana na uongozi wake kutokana  na mgomo aliokuwa nao hivi karibuni ambapo kwa sasa suala limebakia kwa kocha Zahera kuweza kuamua juu ya kumrejesha baada ya kumkataa.

Meneja wa Beno, Seleman Haroub, amesema kuwa kilichobakia kwa upande wao wanasubiria maamuzi ya viongozi wa Yanga ambao wamesema watakutana na kocha kwa ajili ya kuzungumza naye kwa kuwa amemkataa.

“Kama ilivyosikika kuwa mwalimu Zahera amemkataa Beno, hivyo kwa sasa tunausubiria uongozi uweze kuamua juu ya mchezaji huyo kwani walikuwa katika  vikao vyao vya klabu na wakimaliza ndipo  tutakaa kuzungumza suala la Beno.

“Kuhusu kuanza mazoezi kunategemea na maamuzi ambayo wataafikiana uongozi na kocha wao, hivyo  hatujajua nini kitatokea,” alisema, Haroub.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Husein Nyika amesema kuwa mwalimu alikuwa na tatizo na Kakolanya ila muda si mrefu kila kitu kitakuwa sawa.

 “Ndio kweli mwalimu alikuwa na tatizo na Kakolanya, Sisi kama uongozi tutakutana na mwalimu kuweza kulizungumzia suala hilo na mambo yote yatakwenda sawa.” alisema.

Zahera kwa sasa yupo nje ya nchi ambapo alisema kuwa anakwenda kushughulikia masuala yake binafsi na akimaliza atarejea ili kuendelea na majukumu yake ndani ya Yanga.

9 COMMENTS:

  1. Leaders like Nyika should leave Yanga alone. Why should he entertain divisive elements in the team!? Let Kakolanya find a new team. Kocha Zahera amekwishatoa msimamo wake, Montana aseme nini zaidi?

    ReplyDelete
  2. Nyika nashangaa mpka Leo unasubiri nn yanga kwa madudu yote umefanya. Mpka ufukuzwe kwa fimbo au utishiwe kupigwa mawe? Kama unajielewa ungesepa tu yanga hatukutaki tapeli wewe

    ReplyDelete
  3. MKimwacha simba mwenye njaa yupo kinywa wazi ni haki yake ya msingi kudai chake na soo usalitu

    ReplyDelete
  4. Mimi nakubaliana na suala la kakolanya kurudi ila kwa sharti moja tu, aombe msamaha coach, viongozi pamoja na cc mashabiki ambao daima tulimpenda sana lakini akatutia nyongo ghafla. akifanya hivyo arudi na aanzie bench kwani Kindoki na Kabwili wana uchungu na timu ndo maana wapo hata kwa mvua au jua. Uwezo wa Kindoki ulifichwa na Kakolanya ila ni kipa mzuri kama si yy tunge draw na african lyon.

    ReplyDelete
  5. Replies
    1. DHAMBI HII TUNAYOIFANYA NI KUBWA. MTU ANADAI PESA YAKE HALIPWI, AMEAMUA KUKAA PEMBENI, ANATAKIWA YEYE NDIYE AOMBE MSAMAHA? BASI MLIPENI KWANZA

      Delete
    2. Kwahiyo ameshalipwa hadi anaamua kurudi?

      Delete
  6. Na hatutakubali hili Swala limgeukie kocha wetu kipenzi,Zahera!

    Hiyo kocha ni chachu yq mabadiliko siyo mnafiki analijua soka halihitaji blabla ni hazina so Nyika usepe tuachie timu yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic