December 22, 2018


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima amefunguka kwamba kocha wake, Mbelgiji Patrick Aussems  amemwambia ataanza kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara katikakikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na kuelewa juu ya uwezo wake.

Niyonzima amekuwa na wakati mgumu wa kupangwa katika kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na uwepo wa viungo wengi akiwemo Claytous Chama, Hassan Dilunga ambao wamekuwa wakianza kwenye kikosi cha timu hiyo.

Hivi karibuni Niyonzima aliiongoza Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara mbele ya KMC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

“Kocha ameniambia kwamba anaelewa juu ya uwezo wangu na karibuni tu ataanza kunianzisha kwenye kikosi cha kwanza, hivyo ni kazi yangu kuendelea kujituma  zaidi ili kumfanya anipe namba katika timu hiyo.”alisema.



3 COMMENTS:

  1. Mungu atakusaidia nasi tunakuombea nawe ujitahidi zaidi hasa maelezo ya kocha

    ReplyDelete
  2. Uko sawa kocha tu anajitera mwenyewe,na wewe mwenyewe ulivyozingua mwanzo dah ndio hivyo tena,ila mlpambana na hali yako mbona unampoka mtu namba muda si mrefu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic