YANGA YAILAZA RUVU SHOOTING 3-2 DAKIKA ZA MWISHO TAIFA
Kikosi cha Yanga kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga imejipatia mabao yake kupitia kwa Amis Tambwe, Feisal Salum na Heritier Makambo aliyefunga kwenye dakika za mwisho kabisa za mchezo.
Wapinzani wao Ruvu Shooting, walifanikiwa kupata mabao yao kupitia kwa Fully Maganga na Said Dilunga aliyefunga kwa mkwaju wa penati.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga izidi kujiweka kileleni kwa kuwa na alama 44 na kuiacha Azam yenye 40 kwenye nafasi ya pili.
All the best Young African in the race of championship
ReplyDeleteThis is yanga,mna mwendo mzuri sana bado game tatu zikiisha hizo bila kufungwa kombe lenu hakuna mjadala.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete