January 8, 2019


Ni salaam kwa Simba. Klabu ya Al Ahly ya Misri iliyopangwa kundi D na Simba SC ya Tanzania kwenye hatua ya makundi ya CAF Champions League, imekamilisha usajili wa Beki Yasser Ibrahim kutoka Smouha SC.

Ibrahim anayechezea klabu hiyo ya Alexandria, ametia saini ya miaka minne huku dau lililotumika kumnyaka likifichwa.

Beki huyo amekuwa mchezaji wa 6 kusajiliwa na Al Al Ahly kwenye dirisha dogo la usajili wengine ni Angels Giraldo, Mohammed Mohmoud, Mohmoud Wahid, Ramadhan Sobhi na Hussein Al-Shahat.

Usajili huo umekuwa uifanyika kuelekea mechi za hatua ya makundi Africa ambapo wapo kundi moja na Simba ya hapa Tanzania.


5 COMMENTS:

  1. Simba hawapo vizuri kwenye baki yao kitu ambacho hata ukimuuliza mtu asiejua mpira atakwambia hivyo. Hata mechi ya Jana ya mapinduzi cup kati yao na KMKM.beki ilikuwa ya hovyo sema hao wanamaji wa kinzanzibari walikosa kujiamini walipofika langoni kwa Simba la sivyo Simba alikuwa anafuungwa jana. Lakini Simba wenyewe hata habari hawana wamelala usingizi wakisubiri majaaliwa. Hivyo east Africa mzima au Africa Simba wanashindwa kusajili beki wa kuongezea nguvu timu katika hatua ya makundi?

    ReplyDelete
  2. Kwahyo kuna beki isiyofungika hapa duniani kweli? Unataka beki gani aje kucheza simba aisee. Sizani kama nisahihi kusema simba wamelala wakati pale kuna watu wanewekeza pesa zao nyingi na tofauti na sisi ambao tunapiga kelele tu. Naamini wao wanaongea na mwalimu kila siku na ndiye anaweza kuwaambia uimara na udhaifu wa kikosi na siyo sisi tunaosubiri timu uwanjani

    ReplyDelete
  3. Najipa moyo kuwa simba nao watafanya usajili..!
    Hawawezi kufika kokote kwa kikosi walicho nacho sasa!!

    ReplyDelete
  4. Wenzetu wasajili sisi tunaandaa sababu kujitetea tukishafungwa. Ni kweli tumeridhika na kikosi tulichonacho? Tatizo wabongo tunaridhika na mafanikio madogo sana. Sikushangaa Taifa stars ilipocheza na Ivory Coast mchezaji wetu Canavaro alisema baada ya mechi kuwa Drogba ni wa kawaida sana.

    ReplyDelete
  5. Timu ya Simba ni nzuri ndio maana imefanikiwa kufika hatua ya makundi. Kuna upungufu kwenye nafasi ya beki wa kushoto kwani aliyepo anapitika kirahisi, japo ana uwezo wa kusukuma mashambulizi mbele. Mpaka sasa sijui kwanini Asante Kwasi hatumiki kwenye nafasi hiyo. Lakini Kwasi pia angeweza kuziba pengo la Nyoni kama beki wa kati. Amekuwa akicheza vizuri kwenye nafasi hiyo tangu alipokuwa Mbao FC. Kingibe kinachonishangaza ni Simba kutosajili wachezaji wa kuongeza nguvu wakati wa dirisha dogo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic