January 8, 2019


Hii ni sasa kali. Unaambiwa mara baada ya beki kisiki na tegemeo ndani ya kikosi cha Simba, Erasto Nyoni kuumia juzi katika mchezo dhidi ya KMKM wa Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, Kocha Mkuu, Patrick Aussems amesema atapelekea kikosi cha pili.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kuumia kwa Nyoni jambo ambalo limemuumiza Aussems na kuona kama wanaweza wakapata majeruhi wengine kwenye mashindano hayo.

Mbelgiji huyo ambaye Jumamosi ya wiki hii atakuwa kibaruani kukabiliana na SJ Saoura ya Algeria katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ameamua kufanya maamuzi hayo magumu ili kuepuka msala wa kupoteza nguvu kikosini.

Nyoni aliumia katika mechi hiyo ambayo Simba ilishinda kwa mbinde kwa bao 1-0 na kupelekea kutolewa nje kwa machela.

Ripoti kutoka kwa uongozi wa Simba zinasema mchezaji huyo anaendelea vema na tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya huku dawa za kusaidia kupona kwake akiwa ameshapatiwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic