January 8, 2019


Straika matata anayekipiga katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, Mtanzania Simon Msuva, ametoa somo kwa kikosi cha Simba juu ya mbinu za waarabu uwanjani, imeelezwa.

Msuva ameibuka na kufunguka kuwa ni kweli waarabu wana mbinu za kujiangusha lakini vilevile ni wapambanaji ndani ya uwanja.

Taarifa imesea kuwa Msuva amewashauri Simba kujipanga zaidi kutumia vema uwanja wa nyumbani ikiwemo kufunga mabao ya mapema ili kutoa mwangaza mzuri kwao na mgumu kwa wapinzani.

Kauli ya Msuva imekuja kutokana na kundi D ambalo lina timu za AS Vital, Alh Ahly na JS Saoura ambazo zote ni moto wa kuotea mbali.

Ameeleza kuwa waarabu hupoteza muda kwa kujiangusha ovyo-ovyo kama mbinu yao ya kupoteza muda, hivyo ni jukumu la Simba kuwapa ugumu wa kufanya hivyo.

Simba itakuwa inakipiga na JS Saoura kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi ya wiki hii ambapo ndiyo utakuwa mchezo wa mkondo wa kwanza kabla ya kurudiana nao nchini kwao wiki moja baadaye.

3 COMMENTS:

  1. Huu siyo mtoano brother kwa hiyo ukisema simba watarudiana nao wiki moja baadae unapotosha. Baada ya hiyo mechi simba ataenda kucheza na ama Vita au Al Ahly ugenini

    ReplyDelete
  2. "Simba itakuwa inakipiga na JS Saoura kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi ya wiki hii ambapo ndiyo utakuwa mchezo wa mkondo wa kwanza kabla ya kurudiana nao nchini kwao wiki moja baadaye." HIVI HIZI TAARIFA MNAZITOA WAPI? HII NI LIGI KUNA TIMU NYINGINE SIMBA ITACHEZA NAZO KABLA YA KURUDIANA NA JS SAOURA NA HIYO ITAKUWA ZAIDI YA WIKI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic