BAADA YA KUFUTA LESENI YA MASHAMBA ANAYOMILIKI BOSS SIMBA, MAGUFULI AJA NA TAMKO ZITO
Rais John Magufuli amesema yeye ndiye huagiza watu wanyang'anywe mashamba kwasababu anaona kuna watu wengi wanajimilikisha mashamba makubwa na hawayaendelezi lakini wananchi wa maeneo ya jirani hawana ardhi ya kulima
Ameongeza kuwa jambo hili lipo sana mikoa ya Tanga na Morogoro na baadhi ya watu hao hutumia ardhi hiyo kuombea mikopo kwenye benki, wengine mpaka nje ya nchi
Ameitaka Wizara ya Ardhi kuendelea kufanya hivyo kwa yale mashamba ambayo hayatumiki ya mtu yeyote na waendelee kuyaleta kwake naye ataendelea kuyafuta kwa mujibu wa Sheria.
Kauli ya Rais Magufuli imekuja kufuatia serikali kufufuta mashamba sita (ekari 12,915.13) ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL) yaliyopo Korogwe jijini Tanga, kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.
0 COMMENTS:
Post a Comment