Waraka wa Seleman Matola kwa Simba kuelekea kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Vita ya Congo, siku ya Jumamosi:-
AZAM FC mnapaswa pongezi kwa kufanikiwa kulitwaa kombe la Mapinduzi kwa mara ya tatu mfululizo hali inayoonesha kwamba mlidhamiria kufikia malengo yenu ambayo mlikuwa mmejiwekea na hatimaye mmefanikiwa.
Nakumbuka wakati mashindano yanaanza Azam FC kupitia Ofisa Habari wake, Jaffary Maganga alisema kuwa malengo makubwa ya kushiriki katika kombe la Mapinduzi ni kuweka heshima na kufanikiwa kurejea na kombe bara ili liwe lao jumlajumla.
Hicho ndicho kimetokea na wamefanikiwa kutetea ndoto zao na malengo yao ambayo yalikuwa yamebebwa na uhitaji wa wachezaji, mashabiki pamoja na viongozi waliokuwa wameamua kuwekeza nguvu nyingi kwenye mashindano haya.
Nikukumbushe kwamba Azam wanaweka rekodi ya aina yake baada ya kufanikiwa kulitwaa kombe hilo mara tatu mfululizo, walianza kufanya hivyo mwaka 2017 kisha 2018 na wamefanya hivyo mwaka huu 2019 hali ambayo inawafanya wajimilikishe kabisa kombe la Mapinduzi.
Wanarejea wakiwa wamejaa furaha ya ushindi pamoja na mifuko yao kutuna zawadi ya shilingi milioni 15 huku wachezaji wakiwa na medali ya dhahabu, pia mfungaji bora wa michuano ni Obrey Chirwa ambaye ana mabao matano.
Kupitia Azam FC kuna kitu cha kujifunza hasa kwa timu zetu ambazo zinashiriki mashindano mbalimbali kutokana na namna ambavyo wenzetu wamefanikiwa.
Ukiachana na changamoto ambazo wamepitia pamoja na aina ya vikosi walivyokutana navyo bado kuna kitu kipo nyuma ya mafanikio ya Azam FC.
Kwa upande wa waandaaji pia iwe somo kwao hasa kwa kuangalia upepo unavyokwenda na kuyaandaa mashindano katika hali ambayo italeta ushindani.
Kwa sasa mambo mengi yamebadalika na mipango pia inabidi ibadilike ili kwenda sawa na ushindani uliopo kwenye uwanja wa mpira kiujumla bila kumuacha hata mmoja nyuma.
Nasema hivyo kwa sababu miaka ya nyuma ushindani ulikuwa ni mkubwa na timu nyingi ambazo zilikuwa zinashiriki zilikuwa zinanguvu kubwa hali ambayo ilikuwa ni ngumu kuweza kumtambua mshindi.
Kila mmoja alikuwa anapiga hesabu za kuwa bingwa hali ambayo ilifanya kila mchezo kuwa na msisimko wa kipekee.
Tofauti kabisa na mwaka huu ni timu moja tu ambayo ilikuwa inasema hadharani kwamba inahitaji kupata ubingwa huku wengine wakiishia kusema kimyakimya.
Hali hii inaua ushindani na kufanya ule mvuto upungue taratibu kwenye ushindani, baada ya kukamilisha mashindano sasa hesabu kubwa ziwe kuboresha mashhindano haya yawe katika ubora uliozoeleka.
Timu shiriki zote zilikuwa zimebwana na ratiba ya Ligi Kuu huku nyingine zikiwa zinashiriki mashindano ya kimataifa hali ambayo imepelekea kupeleka vikosi vyao vya pili na wengine kushindwa kufika kabisa.
Simba na Yanga hawakuweka nguvu ya kutosha kwenye mashindano haya na ndio maana hata walipopoteza hakukuwa na maumivu makubwa kwao kwani walikuwa wanalinda wachezaji wao waweze kutumika katika mashindano makubwa.
Pia tumeona namna ambavyo yameipa hasara timu ya Simba hasa kwa kupata majeruhi katika mchezo wao hali ambayo ilimfanya kocha mkuu aingiwe na hofu hata kwenye fainali kupeleka muziki mzito.
Somo jipya kwa waandaaji ni kwamba wanapaswa waangalie namna mpya itakayowasaidia waweze kuibuka na mvuto mpya hasa kwa kuanzia na maboresho ya ratiba.
Wakifanikwa kucheza na ratiba itawafanya wawe na uwanda mpana kwa washiriki kuwa huru kucheza kwa ushindani bila kuwa na hofu yoyote kitaifa na kimataifa.
Nikirejea sasa pale kwenye somo ambalo Azam wametoa ni kwamba katika michezo jambo lolote linawezekana endapo kutakuwa na nia moja.
Kama ambavyo Azam FC waliamua kuwa na lengo la kutwaa ubingwa na wakafanikiwa sasa ni zamu ya Simba kuwa na nia ya dhati ya kuvuka hatua ya makundi watafanikiwa.
Wameanza vizuri kwa kupata pointi tatu wakizubaa na kubweteka wataanza kupoteza ile morali ambayo wanayo kwa sasa kwenye mashindano ya kimataifa.
Wasisahau kwamba Jumamosi wanakutana na AS Vita ambao watakuwa nyumbani na wana maumivu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Wachezaji na viongozi wa Simba wabebe falsafa ya Azam na kuamua kwa dhati kwamba wanahitaji kuvuka hatua ya makundi na ili kufanikiwa kwa hilo kazi ni moja tu kushinda.
Timu nyingine pia ambazo zinashiriki mashindano kama ya FA na Ligi lengo lao liwe moja tu kupata matokeo chanya katika michezo wanayocheza.
Licha ya ugumu ambao timu ambazo hazina mdhamini kwa sasa zinapitia bado zina nafasi ya kufanya vizuri endapo zitakuwa na malengo.
Kwenye mpira tunasema kila kitu ni mipango na hesabu kali ambazo zitafanikisha kufikia malengo ya timu pamoja na wachezaji.
Kutoka Championi
Azam hawajui qanachotaka wanachosha kikosi cha kwanza kwa kushiriki kila kombe na kiwachezeaha hao
ReplyDelete