January 11, 2019


MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Alliance, Bigirimana Blaise amesema kuwa ana imani ya kuendelea kufunga mabao zaidi akiwa hapo ili kuisaidia timu yake iwe katika nafasi nzuri.

Blaise kwa sasa amefikisha mabao sita kwenye orodha ya wafungaji amekuwa msaada tangu aliposajiliwa na Alliance akitokea Stand United kwani tayari amefunga mabao mawili katika kikosi chake kipya.

"Tuna kazi kubwa kwa sasa hasa kutokana na ushindani uliopo ndani ya Ligi, naona timu inapambana kupata matokeo na hicho kinatusaidia kutupa nguvu ya kupambana.

"Suala la wakati na kuona ni namna gani tutaweza kutoka hapa tulipo mashabiki waendelee kutupa sapoti watafurahi wenyewe kwani tutafunga sana msimu huu," alisema Blaise.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic