January 11, 2019



UONGOZI wa Simba, ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi Kuu Bara, umesema kuwa katika mchezo wao wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoure ya Algeria hawatakuwa na huruma kwa maharamia watakaouza jezi feki za Simba Uwanjani hapo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wamejipanga kiasi cha kutosha kutoa burudani kwa mashabiki huku wakiwa na jezi zao orijino na sio zile za kuungaunga kwa wale watakaouza jezi feki cha moto watakiona.

"Tuna jezi mpya na orijino kwa kuwa sisi ni mabingwa lazima mipango yetu iwe ya kibingwa, jezi zetu mpya zina nembo maalum kwa ajili ya kudhibiti maharamia wanaotengeneza jezi feki za Simba.

"Hizi jezi zitatumika kwenye michuano hii na kwa sasa zitauzwa shilingi 15,000 tu, mashabiki wetu wanunue hizi na wauzaji wa jezi feki tutakula nao sahani moja kwa sababu tumeunda kamati maalum ya kuwashughulikia, mimi mwenyewe nikiwemo na hatutokuwa na huruma katika hili.” alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic