January 11, 2019



UONGOZI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba umesema hesabu zao kubwa kwa sasa ni kufanikiwa kuvuna pointi tisa za michezo yao yote ya hatua ya makundi zitakazochezwa Uwanja wa Taifa.

Simba wanawakilisha nchi kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika wakiwa kundi D lenye timu kama JS Saoure ya Algeria, Al Ahly ya Misri na AS Vita ya Congo wataanza kazi yao rasmi kesho na waarabu Uwanja wa Taifa wakicheza na JS Saoure ya Algeria.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi sasa lengo lao kubwa ni kushinda mechi zote za nyumbani.

"Tumefanikiwa kutinga hatua ya makundi ulikuwa ni mpango wetu, sasa mpango mpya ni kufanikiwa kuvuna pointi tatu katika michezo yote tutakayokuwa nyumbani ili kujiweka sehemu nzuri.

"Tutakuwa na michezo mitatu nyumbani ambapo tukishinda yote maana yake tuna pointi tisa, baada ya hapo ugenini tunachokwenda kukifanya ni kulazimisha kubeba pointi moja, ndiyo inawezekana kama sera yetu inavyosema, mashabiki watupe sapoti," alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic