January 9, 2019


MAKOCHA wa timu shiriki za Ligi kuu ya wanawake Tanzania wameanza kulalamika juu ya waamuzi wanaochezesha mechi za ligi hiyo maarufu kama Serengeti Women's Premier League wakidai hawafuati sheria 17 za mpira.

Katika ligi hiyo ambayo tayari kila timu imecheza mechi tatu, JKT Queens ni kinara akiwa na pointi tisa, akifuatiwa na Mlandizi Queens, Simba Queens na Siterz FC ambazo zote zina pointi saba.

Kocha wa Tanzanite SC, Abdallah Juma, amesema kuwa, ligi hiyo inaharibiwa na maamuzi mabaya ya waamuzi ambao mara zote wameonekana kuzipendelea baadhi ya timu.

Kocha wa Alliance, Ezekiel Chobanka amesema waamuzi wengi wanashindwa kutoa maamuzi sahihi katika tukio husika hali inayosababisha mizozo ya mara kwa mara na kuibua hisia huenda wanaagizwa kupendelea upande fulani.

Ofisa Habari wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema waamuzi wanaujuzi na elimu ambayo inawafanya waweze kuchezesha Ligi hiyo ambayo ina msisimko hivyo taratibu zitafuatwa kwa wale ambao watafanya makosa cha msingi ni mashabiki kujitokeza kwa wingi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic