January 20, 2019



LIGI Kuu Tanzania Bara leo inaendelea kwa timu kumi kushuka Uwanjani kumenyana ili kupata pointi tatu muhimu.

Coastal Union ya Tanga leo itamenyana na African Lyon kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani, Tanga.

Singida United leo watamenyana dhidi ya KMC, Uwanja wa wao wa nyumbani Namfua, Shinyanga.

JKT Tanzania leo wataikaribisha Mbao FC kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Mej.Gen.Isamuhyo, Dar es Salaam.

Kagera Sugar leo atakuwa na kibarua dhidi ya Biashara United Uwanja wa Kaitaba, Kagera na Alliance FC atamenyana na  Mbeya City Uwanja wa Nyamagana.

1 COMMENTS:

  1. "Singida United leo watamenyana dhidi ya KMC, Uwanja wa wao wa nyumbani Namfua, Shinyanga".
    MWANDISHI! Tatizo ni nini? umakini au kukopy na kupest kumezidi?
    Maana kwanza Singida leo ni wageni wa KMC na sio kwamba wanachezea uwanja wa Namfua.
    Na pili, Uwanja wa Namfua haupo Shinyanga bali Singida. Mnaboa jamani. Mnaonekana kama mnabahatisha tu humu kutuletea taarifa!.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic