January 11, 2019


MAMBO yamezidi kupamba moto kwa wagombea uongozi ndani ya Yanga ambapo mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, Mbaraka Igangula amepania kufanya mambo makubwa iwapo atapewa nafasi hiyo kwa kuijenga upya Yanga.


Igangula amesema kuwa ataanza kuweka nguvu kwenye Kamati ya Usajili wa Yanga baada ya kubaini kwamba kuna mambo mengi ya ovyo ambayo yanafanyika na kusababisha kuwakosa wachezaji muhimu ndani ya Yanga.

"Nikipewa mamlaka haya ndani ya mwaka mmoja nitaweka sawa mipango mingi ndani ya Yanga kwa kuanza na kamati ya Usajili kwa kuwa Yanga ni klabu kubwa na haipaswa kumkosa mchezaji yoyote yule ila kwa sasa viongozi ambao wanaiongoza idara hii wamekuwa wakiiendesha kwa maslahi yao.

"Hatuwezi kukubali watu watumie mpenyo huu wa usajili kuyajaza matumbo yao mimi siwezi kukubali kabisa nitapambana nao kuweka usawa kwa maendelo ya Yanga," alisema.

Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi za viongozi wa Yanga kwa kuanzia ngazi ya Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti na Wajumbe watatu.

2 COMMENTS:

  1. Watu wanatumiwa kutaka kuidhoofisha Yanga....wameona Yanga inataka kusimama Imara...wanaona umoja wa wanayanga walikuwa wapi siku zote mpaka Ijumaa leo....lakini Yanga itaendelea kusimama imara pamoja na yote haya!

    ReplyDelete
  2. Kwahiyo baada ya hizo kesi za kuzuia uchaguzi kuchaguliwa, maana yake Manji anarudishwa....vyovyote vile itakavyokuwa Yanga inaonekana ni Imara....Manji anaendelea kusaidia Timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic