January 11, 2019


KOMBE la Mapinduzi leo linaendelea ikiwa ni hatua ya nusu fainali ambapo timu nne zitamenyana katika Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar kumtafuta mbabe atakayetinga hatua ya Fainali.


Nusu Fainali ya leo itaanza saa 10:15 kwa mabingwa watetezi Azam FC kumenyana na KMKM huku Simba na Malindi wakimenyana saa 2:15 Usiku katika Uwanja wa Amaan.

Simba ni vinara wa kundi A wamekusanya pointi tisa baada ya kushinda michezo mitatu wakifuatiwa na Mlandege wenye pointi nne na Azam FC wanaongoza kundi B wakiwa wamekusanya pointi 10  wakifuatiwa na Malindi wenye pointi saba baada ya kucheza michezo minne.

Vinara wa mabao katika kombe la Mapinduzi ni Obrey Chirwa wa Azam FC na Abdulswamadu Ali wa Malindi wote wakiwa na mabao matatu, fainali ya kombe hili itachezwa Januari 13.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic