Nahodha wa timu ya Stand United, Jacob Massawe ameonyesha thamani yake mbele ya wapinzani wao wa muda mrefu Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Uwanja wa Kambarage.
Masawe alifunga bao pekee na la ushindi dakika ya 88 kwa kichwa akitumia makosa ya mabeki wa Yanga ambao walimpa nafasi ya kupiga kichwa kilichompoteza Klaus Kindoki.
Licha ya Yanga kuongoza kwa kumiliki mpira walishindwa kutibua mipango ya Stand United,' Chama la wana' walifanikiwa kulinda ushindi wao.
Stand United wanafanikiwa kuvunja rekodi ya Yanga baada ya kucheza michezo 19 bila kupoteza leo wanapoteza mchezo wa kwanza wakiwa ugenini kwa bao la usiku.
Raha ya kuchezea nje ya Dar!
ReplyDeleteSasa wimbo wa viporo...viporo utasikika!kama kwamba mwaka juzi na Jana wao walikuwa hawana viporo!
ReplyDeleteMwabeja sana shinyanga! Bado Mwanza na Musoma...Kanda maalumu
ReplyDeleteKwani kumetokea nini?
ReplyDeleteNasikia vigelegele mwali kabikiriwa nini?
Ha ha haaaaaaaaaa, imenifurahisha saaaaana! "Mwali Kabikiliwa" huyo atakuwa ni "Bikra Kidawa".
DeleteYeah mwali wamefanywa mbaya na vibonde vilivyo nafasi ya 16...afadhali mikia fc walitendwa na walio nafasi ya 5!
ReplyDeleteHuyu jamaa yanga isipofanya vizuri hatumi habari kwawakati,kulikon?
ReplyDeleteSaleh jembe ndivyo walivyo..wakifunga Yanga wanaweka matokeo fasta hata iwe mechi ya SAA mbili usiku..Ikicheza simba usiku ikashinda unakuta had SAA tano asubuhi Sikh inayofuata hawajaweka matokeo..jifunzeni kwa bin zuberi.sio sawa kuegemea upande mmoja
DeleteHas saleh jembe kulikoni...kichwa cha habari hapo kinaonyesha mlikuwa mnafuatilia mechi!mbona matokeo hamweki..
ReplyDeleteAngekuwa Makambo kafunga hapo mngekuwa mmeweka..zaidi ya nusu SAA tangu mechi imeisha...Bin zuberi keshaaandika..".Wametobolewa"
ReplyDeleteSio nusu saa tu, pale pale goli linapofungwa utasikia "kwasasa ni dakika ya 75 Makambo anaitanguliza Yanga kwa Goli la kibabe!". Yaani hapo kila dakika inapobadilika utapata taarifa hadi dakika ya 90. Utasimuliwa hadi faulo zote na kona zote na dakika zake!
DeleteBlog hii mimi mwisho leo.Shafi Dauda alianza hivi hivi blog imemfia mkononi. Hakuna wasomaji.
ReplyDeleteHii nayo imeanza kuleta chuki nä habari za upande mmoja dawa ni kuisusa.