YANGA YACHEZESHEWA PATA POTEA SHINYANGA, YAKUBALI KICHAPO CHA BAO 1 MTUNGI
Kikosi cha Yanga kimekubali kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara katika mchezo uliopigwa CCM Kambarage Shinyanga dhidi ya Mwadu FC kwa bao 1-0.
Bao pekee la mchezo huo limewekwa kimiani na Jacob Masawe mnamo dakika ya 88 ya mchezo kunako kipindi cha pili.
Ushindi wa Stand unaifanya Yanga iendelee kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama zake 53 ikiwa imeshacheza michezo 20.
Katika msimu huu tangu kuanza, Yanga ilikuwa haijapoteza mchezo wake hata mmoja zaidi ya kwenda suluhu na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo pia yanaifanya Stand kufikisha alama 25 ikicheza jumla ya mechi 23 mpaka sasa.
Wametobolewa!
ReplyDeleteNa bado Mbao Mwanza!
ReplyDeleteInginia somaaaa!!!!!
ReplyDeletehongera sana jacobo massawe kwa kupeleka kilio jangwani, hongera chama la wana.
5 G, wadosi wanaita punch...
DeleteSomeni kule Kinshasa
ReplyDeleteAfadhali hao wamefika makundi Kinshasa.. Miaka yote Yanga walikuwa wanaishia wapi?
DeleteKikotoo kipya kimewabeba, kingetumika cha zamani mngeishia njiani kitambo...
Deleteila mlijitapa sana, mpira sio taarabu
Afadhali kufungwa 5 na Vita kuliko kufungwa 1 na timu ya 16 kwenye ligi ya Bongo.
ReplyDeleteKufeli chekechea na kufeli kidato cha 4 ipi aibu?
ReplyDeleteMatundu 5 mengi...
Bado yale ya Mashujaa, hivi wapo nafasi ya ngapi TPL?
Kwa hiyo unajua nani yupo chekechea na nani yupo form 4.
ReplyDeleteKwa hiyo hawalingani.
Nyie bado mnanuka maziwa.Malindi wapo wa ngapi vile?
Nasikia mnataka Kakolanya arudi.Bikra ndio imevunjwa na Stendi sasa kila mmoja atajilia tu.Subiri uone.
Mwandishi, check paragraph ya kwanza, sio Mwadui ni Stand ndio waliotoa bikra ya mtu. Sasa hapo Stand wameshang'oa Koki, subiri uone maji yatakavyomwagika. Mlipohesabu mechi nne za ubingwa, hii ya stand hamkuihesabu. Kwahiyo zimebaki nne zilezile.
ReplyDelete