KOCHA wa Mbao FC, Ally Bushiri amesema ushiriki wa timu yake katika michuano ya SportPesa Cup kwa mara ya kwanza kumeikomaza timu na kuifanya iongeze uwezo wa kujiamini kutokana na ushindani aliokutana nao ndani ya mechi tatu alizocheza.
Bushiri amesema nafasi aliyofikia si mbaya kwani alicheza na timu bora Simba hali iliyomfanya atumie nguvu nyingi kujilinda na katika hilo amefanikiwa na kushindwa kwake kwa penalti ni hatua kubwa.
"Vijana wamejifunza, wameonyesha ushindani na wamecheza na timu kubwa na bora, kwa hapa tulipofikia si hatua mbaya kwani ni mwanzo, imani yetu ni kuendelea kuleta zaidi ushindani katika mashindano mengine.
"Kwa moyo wa dhati nawapongeza Simba kwa ushindi wao wa leo wamecheza kwa juhudi nasi tumecheza ila kwenye fainali mshindi lazima apatikane," alisema Bushiri.
Mbao FC wamefanikiwa kuandika rekodi mpya kwenye michuano hii baada ya kuvunja utawala wa Gor Mahia kutwaa kombe mara mbili mfululizo pamoja na kuwafunga bao kwa mara ya kwanza ndani ya dakika tisini kwani katika michezo waliyocheza ya SportPesa Cup tangu 2017 na 2018 hawajawahi kufungwa ndani ya dakika 90.
Mbao walicheza Team work, Simba walicheza Individual work, hapo ilikua ni Team VS Wachezaji
ReplyDeletemichuano hii imeonesha kwamba vijana wadogo wanafundishika kucheza kitimu tofauti na wakongwe ambao hucheza kiuzoefu
ReplyDeleteThat is football maturity!
ReplyDelete