KIKOSI cha KK Sharks kutoka Kenya leo kimetwaa ubingwa wa SportPesa Cup baada ya kushinda mchezo wa fainali dhidi ya Bandari kwa ushindi wa bao 1-0 uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Bao pekee lililofungwa na Mwenda Harison aliyefunga kipindi cha pili dakika ya 60 lilidumu mpaka mwisho wa kipindi licha ya Bandari kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Kwa ushindi huo KK Sharks wanapewa zawadi ya dola 30,000 pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi cha Everton ya England.
Mshindi wa pili wa mashindano haya ni timu ya Bandari huku mshindi wa tatu akiwa ni Simba kutoka Tanzania.
Hii ni mara ya tatu kwa timu za Kenya kutwaa taji la michuano ya SportPesa Cup na ni mara ya pili kuchukua katika ardhi ya Tanzania na bingwa mtetezi Gor Mahia ya Kenya alitolewa na Mbao FC hatua ya robo fainali.
safi sana maana huyu kocha wa bandari alianza kuleta mambo ya usimba na yanga
ReplyDelete