LEO ni fainali ya kombe la Mapinduzi ndani ya Uwanja wa Gombani uliopo Pemba, Zanzibar, Simba na Azam mzigoni.
Fainali hizo zitafanya kupatikana kwa bingwa mpya wa kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2019, maswali yatajibiwa kama Azam atabeba tena mara ya tatu ama Simba atachukua leo.
Azam FC wao wanatamba kwamba ni kikosi bora na mabingwa watetezi wa kombe hilo la Mapinduzi huku Simba wao wakijita wazee wa kikosi kipana nao hesabu zao ni kutibua mipango ya Azam, hizi hapa dondoo muhimu za timu hizi kabla ya fainali ya leo.
Kuhusu Ubingwa.
Timu zote mbili zimetwaa ubingwa huo mara tatu , Azam FC wamefanikiwa kutwaa kombe hilo, 2012, 2017 na 2018 hivyo ni mabingwa watetezi wanalihitaji ili walibebe jumlajumla.
Simba wao wamebeba mara tatu pia walianza mwaka 2008, 2011 na 2015 hivyo leo itakuwa ni fainali ya kisasi kwa kuwa wanakumbukumbu ya kufungwa mwaka 2018 na Azam bao 1-0.
Makundi yalikuaje
Simba wao walikuwa kundi A ambalo lilikuwa na timu nne kama Mlandege, KMKM na Chipukizi.
Azam wao walikuwa kundi B ambalo lilikuwa na timu tano kama Malindi, Yanga, Jamhuri na KVS katika hizi timu Yanga ilikuwa ya kwanza kuondololewa kwenye hatua ya makundi.
Michuano hiyo ilianza Januari 1 mwaka huu Azam FC alicheza Januari 2 dhidi ya Jamhuri walitoka sare ya bao 1-1, Januari 5 akacheza na Yanga akashinda mabao 3-0, kisha KVS alishinda kwa mabao 2-1, Malindi akashinda kwa mabao 2-1 nusu fainali akacheza na KMKM akashinda mabao 3-0.
Simba wao kundi lao A walianza Januari 4 na Chipukizi walishinda mabao 4-1 kisha akacheza na KMKM akashinda bao 1-0 na mchezo wake wa tatu akacheza na Mlandege akashinda bao 1-0 nusu fainali akacheza na Malindi akashinda kwa penalti 3-1.
Aina ya mabao
Simba wamefunga mabao matano kwa kwa mikwaju ya penalti mpaka sasa ikiwa ni bao moja katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Chipukizi, bao la ushindi katika mchezo wao dhidi ya Mlandege na kwenye nusu fainali dhidi ya Malindi wakashinda mabao 3-1 jumla mabao matano.
Azam FC wana bao moja la penalti ambalo liilifugwa kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri.
Uzoefu wa makocha
Mholanzi Hans van Pluijm amekuwa na nafasi nzuri ndani ya ardhi ya Tanzania kutokana na uzoefu wake wa muda ndani ya Ligi Kuu pamoja na kuwa na benchi la ufundi pana kwani ana Juma Mwambusi pamoja na Iddy Cheche ambaye alichukua kombe la Mapinduzi mwaka 2018 hivyo ana mbinu nyingi.
Mbelgiji Patrick Aussems wa Simba ni mara yake ya kwanza kufika hatua ya fainali ya kombe la Mapinduzi anajua namna ya kucheza na wachezaji wake pamoja na mabadiliko ya ufundi.
Uwezo wa Kufunga
Azam wamekuwa bora ndani ya dakika tisini kwani katika michezo mitano waliyocheza ni mchezo mmoja dhidi ya Jamhuri wameshinda Kwa penalti huku michezo minne wakimaliza bila penalti tofauti na Simba ambao katika michezo minne waliyocheza michezo miwili wameshinda kwa penalti ikiwa ni dhidi ya Mlandege na ule wa Malindi.
Mabao ya kufungwa
Azam katika michezo mitano wamefanikiwa Kufunga mabao 11 inanamaanisha safu yao ya ushambuliaji ina uchu wa mabao huku Simba katika michezo 4 waliyocheza wana mabao 9 hali inayofanya safu yao kusumbuliwa na ubutu.
Mabao ya kufungwa
Azam wamefungwa mabao matatu katika michezo mitano, wana safu bora ya ulinzi pamoja na mlinda mlango mwenye uzoefu Razack Abarola, huku Simba wakifungwa mabao 2 katika michezo minne waliyocheza, wana safu ya ulinzi makini ila tatizo lao kubwa lipo kwenye umaliziaji.
Nusu fainali
Azam FC walicheza na KMKM ya Zanzibar na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao matatu ndani ya dakika tisini.
Simba walicheza na Malindi nayo ya Zanzibar ila dakika tisini walikamilisha bila kufungana hali iliyopelekea mwamuzi kuamua ipigwe mikwaju ya penalti wakafanikiwa kushinda Kwa penalti 3-1.
Vita ya ufungaji
Safu ya Azam FC imekuwa haimtegemei mshambuliaji mmoja kila mchezaji anafunga Kwa nafasi yake Ila kinara wa mabao ni Obrey Chirwa ambaye mpaka sasa ana mabao matatu akifuatiwa na Donald Ngoma ambaye ana mabao mawili.
Simba wamekuwa na tatizo la kumtegemea mshambuliaji mmoja anayeandaliwa kuibeba timu ndio maana wamekuwa wakipata taabu kupata matokeo, Meddie Kagere ana mabao mawili huku wengine kama John Bocco Rashid Juma Haruna Niyonzima wana bao moja.
Kutoka Spoti Xtra
0 COMMENTS:
Post a Comment