MCHEZO wa kundi B wa kundi la Mapinduzi kati ya Yanga na Malindi umemalizika kwa Malindi kufanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Yanga, katika Uwanja wa Amaan, Visiwan Zanzibar.
Matheo Anthony alikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza kwa Yanga akiwa ndani ya18 kwa kumalizia kona kwa kisigino.
Dakika ya 41 Malindi walifanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Abdul Swamad Ali akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Yanga.
Dakika ya 62 Hamis Musa alimtengea pasi Juma Boluna akafanikiwa kuandika bao la pili la ushindi.
Dakika ya 62 Hamis Musa alimtengea pasi Juma Boluna akafanikiwa kuandika bao la pili la ushindi.
Mashabiki wa Yanga wamekaa jukwaa moja na wale wa Malindi kutokana na utamaduni wa visiwani Zanzibar tofauti na ilivyo Dar es Salaam.
Mita 40 zile
ReplyDeleteWanaume hao wanarudi Dar!
ReplyDeleteMigongo wazi boti la Kilimanjaro linawahusu.Lakini vyura asili yao maji .
ReplyDeleteHamna cha wanaume wala wavulana .
Eti Cannavaro "timu yenyewe imebaki Dar!" Ni nani aliwaambie muiache Dar?
ReplyDeleteHivyo ni visingizio tu! Kila timu hutoa vyake ikifungwa..Simba walipoondolewa na Mashujaa walidai eti sio kikosi cha kwanza kilicheza..Jana Liverpool imepigwa na wolves wanadai walichezesha watatu ambao ni under 18.Hakuna timu ambayo wanahitaji Mil 15 kuzidi Yanga.Wangepeleka kikoosi cha kwanza wangeweza kuzipata kuliko kutembeza kopo unaishia laki 9 katika mwezi mmoja
Ule wimbo wa Mashujaa hautasikika tena. Kwanza michuano ya Azam Federation cup bado sana
ReplyDelete