January 11, 2019


KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza kuusimamisha Uchaguzi Mkuu wa Yanga uliopangwa kufanyika Jumapili hii kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo imefikia hatua hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa baadhi ya wanachama wa Yanga wamefungua kesi mahakamani wakitaka uchaguzi huo usimamishwe.

Akitangaza uamuzi huo, mwenyekiti wa kamati hiyo, Malangwe Mchungahela, amesema: “Leo tulikuwa kwenye vikao vya mwisho kuangalia kama mambo yote yamekaa sawa.

“Tukiwa kwenye vikao hivyo, tukapata taarifa kwamba kuna baadhi ya wanachama wa Yanga wamefungua kesi ya kusimamisha uchaguzi hapa Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Morogoro na sehemu nyinginezo.

“Sasa sisi kama kamati hatutaki kugombana na muhimili wa mahakama na kwa sababu tumesikia sehemu zingine mashauri yameanza kusikilizwa, tumeamua kusimamisha uchaguzi usifanyike Jumapili hii mpaka tupate muongozo wa kilichojiri huko mahakamani.

“Jumatatu tutawapa msimamo wa uchaguzi, lakini kwa sasa kamati ya uchaguzi imesitisha uchaguzi huo kwa muda na wala hatujaufuta. Wale wagombea waliokuwa wakipiga kampeni tumewaambia wasimame kwanza.”

Uchaguzi huo wa Yanga ulikuwa na lengo la kujaza nafasi za uongozi klabuni hapo zilizoachwa wazi ambapo ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe watatu.

5 COMMENTS:

  1. Watu wanatumiwa kutaka kuidhoofisha Yanga....wameona Yanga inataka kusimama Imara...wanaona umoja wa wanayanga walikuwa wapi siku zote mpaka Ijumaa leo....lakini Yanga itaendelea kusimama imara pamoja na yote haya!

    ReplyDelete
  2. kwa hiyo Manji anarudishwa....vyovyote vile itakavyokuwa Yanga inaonekana ni Imara

    ReplyDelete
  3. sasa nyinyi TFF mmepata barua ya kusimamisha uchaguzi kutoka mahakamani ,au ndio mmesikia tu km mnavyo sema ,acheni ubabaishaji bhanaa

    ReplyDelete
  4. Haya niliyahisi baada ya Kaptein Mkuchika kuthibitisha Manji atarudi kazini..wanachama wanampenda Manji ksbb aliipeleka time mbali..Mkuchika amenyamaza..TFF wanajichanganya..BMT kimya..Wizara kimya..time za wanachama ziachwe wanachama wafuate katiba yao..kama itavunjwa ndo serikali iamue..haya povu la Mchungahela na Mh Waziri..Kiko wapi..uchaguzi umeahirishwa..mbaya Sana..

    ReplyDelete
  5. Hahaha na bado mlianza kwa mikwara ya maagizo sasa wapi mmechemka.Hii ni timu ya Wananchi acheni tuamue wenyewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic