January 11, 2019


MLINDA mlango wa kikosi cha Yanga, Ramadhani Kabwili amesema anafurahi kuona anapata nafasi ya kutumikia kikosi chake hali inayomfanya apambane zaidi kwa kufanya mazoezi.

Kabwili amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera baada ya kuingia kwenye mgogoro na Beno Kakolanya, amesema anatambua shauku ya mashabiki ni kuona timu inafanya vizuri na wanashirikiana na wachezaji wenzake kupata matokeo.

"Tunashirikiana na wachezaji tukiwa Uwanjani hata nje ya Uwanja ili kufanikiwa kupata matokeo, tunajua tuna kazi ngumu mbele ila yote yanawezekana kwani penye nia pana njia, kikubwa sapoti kutoka kwa mashabiki," alisema Kabwili.

Leo ni siku yake ya mfanano ya kuzaliwa, mbali ya kudaka anapenda pia kusikiliza muziki mzuri wa Tanzania pamoja na ule wa kimataifa leo atakuwa nyumbani na jamaa zake.

5 COMMENTS:

  1. Yanga kuweni macho kuna hujuma

    ReplyDelete
  2. Watu wanatumiwa kutaka kuidhoofisha Yanga....wameona Yanga inataka kusimama Imara...wanaona umoja wa wanayanga walikuwa wapi siku zote mpaka Ijumaa leo....lakini Yanga itaendelea kusimama imara pamoja na yote haya!

    ReplyDelete
  3. Watu wanatumiwa kutaka kuidhoofisha Yanga....wameona Yanga inataka kusimama Imara...wanaona umoja wa wanayanga walikuwa wapi siku zote mpaka Ijumaa leo....lakini Yanga itaendelea kusimama imara pamoja na yote haya!

    ReplyDelete
  4. kwa hiyo Manji anarudishwa....vyovyote vile itakavyokuwa Yanga inaonekana ni Imara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic