KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems ameshangazwa na ubutu wa safu ya ushambuliaji yake ndani ya dakika 90 kwa kushindwa kufunga mabao katika mchezo wao wa jana mbele ya Mbao FC.
Simba alicheza na Mbao katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambapo ndani ya dakika 90 hakuna timu iliyoweza kufunga licha ya kutengeneza nafasi nyingi.
Aussems amesema walipaswa wafunge mabao zaidi ya matano kutokana na nafasi walizotengeneza ila walishindwa kwa kukosa umakini uwanjani.
"Sio jambo nzuri kwangu maana wachezaji wangu wamecheza vizuri na wametengeneza nafasi nyingi wameshindwa kuzitumia hili ni tatizo kubwa ambalo natakiwa kulifanyia kazi.
"Kila mmoja ameonesha uwezo wake ndani ya kikosi ila kwa namna walivyopoteza nafasi si jambo la kufurahisha, wachezaji walishindwa kuwa na morali nzuri hali inayonifanya nianze upya kuwajenga warejee kwenye ubora wao," alisema Aussems.
Simba alishinda mchezo huo kwa penalti 5-3 na kuwafanya wawe washindi wa tatu wa mashindano hayo huku bingwa akiwa ni KK Sharks wa Kenya akifuatiwa na Bandari ambaye ni mshindi wa pili.
Hii #Simba isipokaa chini na kujitafakari... Yaani viongozi wa juu wasipotoa karipio kali na msisitizo wa thamani ya jezi ya #Simba sidhani kama watafika mbali..
ReplyDeleteNatarajia viitishwe vikao vya ndani na watu kadhaa akiwemo makocha, manahodha na wachezaji wote kuwekwa kitimoto!!
Lingine muhimu kulifanya mapema ni nafasi ya #Haji Manara ndani ya #Simba.. Yeye kama msemaji wa timu ni amekuwa sehemu ya kueneza propaganda za kusadikika.. Wapo wanaomuamini na kuvimba kichwa kwa maneno yake ambayo kwa asilimia kubwa hayana utaalamu wa aina yoyote!!
#Simba ijitambue mapema la sivyo Waarabu watajipigia mabao mengi tu..!!
bakuunga mkono
DeleteWewe acha kuandika pumba zako.Manara anafanya kazi zuri kwa klab yetu asingekuwa yeye hungeijua ssc wewe achana na simba
ReplyDeleteKuna watu ni mashabiki, lakini hawajui majukumu ya watu ndani ya klabu. Manara yupo pale Simba sio kucheza bali kazi yake ni kuitangaza Brand ya Simba. Huwezi kuitangaza Simba kama hautaisifia Simba, kama hautawasifia wachezaji. Na huwezi kuwa Msemaji wa klabu kama hujaisemea klabu yako mambo mazuri na kuyatangaza malengo mliyojiwekea. Na siku zote malengo ni muhimu yatimie na sio lazima kutimia.
ReplyDeleteHivyo, kwa Manara anachokisema ndani ya Timu mara nyingi ni Umuhimu wa kutimiza malengo, lakini kutimiza malengo hayo sio lazma kwakuwa timu ipo kwenye mashindano na mashindano hatupo Simba peke yetu, na hao nao tunaopambana nao nao pia wanataka kufanikiwa vilevile.
Kwahiyo, wanaomlaumu Manara wanakosea sana, Manara pale yupo kazini, na ule ndo utekelezaji wake wa majukumu yake. Ni lazma aisemee klabu yetu na pia ni lazima aipambe klabu. Nina imani bila Manara hata mapato ya mlangoni pale Taifa yangekuwa hayapatikani kama yale yaliyopatikana kwa mechi nyingi za kitaifa na kimataifa wakati Simba ikicheza. Simba tunaweza, kufungwa ni sehemu ya matokeo, ila pia na Uongozi unatakiwa kuwa karibu na timu kwa nyendo nyingi ambazo zinaweza kuleta matokeo hasi, mfano kwa kitendo cha kumwacha Kocha pekee na timu kambini hadi kupelekea wachezaji kuondoka kambini huku wakijua kesho kuna mechi.