LICHA ya kushindwa kutwaa ubingwa wa kombe la SportPesa Kocha wa Mbao FC, Ally Bushiri amesema kikosi cha Mbao kinastahili pongezi kutokana na kupambana kufika nafasi ya nne.
Mbao ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii waliweza kuwavua ubingwa mabingwa watetezi Gor Mahia katika mchezo wa hatua ya robo fainali kwa penalti 4-3.
Bushiri amesema alikaa na wachezaji wake na kuwapa mbinu mpya ambazo zimewasaidia kupambana licha ya kushindwa kutwaa ubingwa.
"Tumealikwa msimu huu na ni mara yetu ya kwanza tumeona namna ushindani ulivyo, vijana wangu wamecheza mpira kwa nidhamu na wanastahili pongezi licha ya kushindwa kutwaa kombe.
"Michezo mitatu ambayo tumecheza ilikuwa na ugumu wake na kwenye mpira lazima kukubali matokeo, tumejifunza na tutaendelea kupambana," alisema Bushiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment