January 7, 2019


MSHAMBULAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa ameendeleza moto wake wa kucheka na nyavu baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika za lala salama baada ya dakika 90 kukamilika kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar leo.

KVS walikwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 16 lililofungwa na Amour Bakari Ali dakika ya 16 kipindi cha kwanza lililowafanya Azam kusubiri kupindua meza kipindi cha pili.

Bao la kusawazisha la Azam lilifungwa na Donald Ngoma dakika ya 75 na kuweka usawa kwa timu zote na katika dakika za nyongeza Chirwa alifunga bao la ushindi na kufanya Azam washinde kwa mabao 2-1.

Chirwa anakuwa ni kinara wa mabao kwa sasa akiwa amefikisha mabao matatu kwenye mashindano ya Mapinduzi akifuatiwa na Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic