January 13, 2019








Tamasha la Tuzo za Sinema Nchini lijulikanalo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) limezinduliwa rasmi usiku wa kuamukia jana Jijini Dar es salaam.


Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Sinema ulipo jengo la City Mall katikati ya jiji la Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Balozi wa Kenya hapa nchini, Dan Kazungu.


Katika uzinduzi huo, baadhi ya wageni waalikwa walipata nafasi ya kuangalia sinema ya kutoka hapa nchini iitwayo Red Flag ambayo imeigizwa na Mtanzania, Rammy Galis.


Sinema hiyo ndiyo sinema pekee ya kutoka Tanzania ambayo itashindanishwa na sinema nyingine 31 kutoka mataifa mbalimbali ambayo yapenga hatua katika tasnia ya sinema.

Rammy Galis amepata shavu hilo kutokana na sinema yake hiyo kudaiwa kikidhi viwango vya kimataifa kutokana na kutumia Lugha ya Kiingereza.
                                                                                              
 Mkuu wa Uendeshaji wa Azam Media, Yahya Mohammedi, alisema kuwa wanajivunia namna tamasha la SZIFF lilivyoamsha ari na hamasa kwa waandaaji na wapenzi wa filamu nchini lakini pia ni moja ya njia kubwa ya kuzitangaza filamu za Tanzania kimataifa kupitia Televisheni.

“Pia katika tamasha hilo tuna mpango wa kualika mabalozi pamoja na waandaaji maarufu wa sinema kutoka mataifa mbalimbali yaliyopiga hatua ili waje kuangalia filamu zao zikitathiminiwa na Watanzania.




“Kwa hiyo, niwaombe tu wadau wa sinema kutoka hapa nchini watumie tamasha hilo pia kwa ajili ya kujifunza  mambo mbalimbali yatakayowawezesha kuandaa filamu zitakazokuwa zikikidhi viwango vya kimataifa,” alisema Mohammed.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic