Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema baada ya majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wao dhidi ya KMKM, Nyoni alikimbizwa hospitali kufanyiwa vipimo na jopo la madkatari ambao wamegundua tatizo alilonalo sio la kutisha.
"Nyoni ni beki wetu na mchezaji wa kimataifa, kwa sasa anatibu majeraha yake ambayo aliyapata wakati kikosi chetu kikiwa kwenye kombe la Mapinduzi Zanzibar, ila baada ya uchunguzi anachotakiwa kwa sasa ni kupewa mapumziko ili arejee kwenye ubora wake.
"Hatafanyiwa upasuaji wowote atafanya mazoezi maalumu ya kumrejesha kwenye ubora, tunatarajia kama itakuwa kama ambavyo wataalamu wametueleza ataonekana Uwanjani mwezi ujao," alisema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment