WANACHAMA wa Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni za uchaguzi ambazo zimezinduliwa rasmi leo katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na viongozi wa Yanga pamoja na wale wa TFF kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi kuanzia ile ya Mwenyekiti iliyokuwa wazi baada ya Yusuf Manji kujiuzulu pamoja na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine.
Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13 katika ukumbi wa Polisi Messi Oysterbay kuanzia saa moja kamili asabuhi, huku wanaotakiwa kufanya uchaguzi huo wakiwa ni wanachama hai wenye kadi za kitabu pamoja na zile za benki.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo, amesema wanachama wanatakiwa waheshimu taratibu zilizopo kwa kufuata sheria na kufanya kampeni zilizo salama bila kujihusisha na masuala ya uchochezi.
"Utaratibu upo wazi na kampeni zifanyike kwa amani bila bugudha yoyote kwa sababu lengo letu ni kupata viongozi bora na si bora viongozi.
"Wale wanachama ambao wanatisha wengine ama wale wenye hisia za kufikiria kuhusu migogoro hao wanapswa waelewe kwamba sheria inafanya kazi na watakaojihusisha kwenye vurugu hatua kali juu yao zitachukuliwa," alisema Siza.
Mwenyekiti wa uchaguzi wa Kamati ya TFF, Mchungahela Ali amesema kuwa wamejipanga vizuri kwa wale ambao wamejipanga kufanya vurugu ama kupinga kampeni hatua kali juu yao zitachukuliwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment