January 18, 2019



KOCHA Mkuu wa timu ya Azam FC, Hans Pluijm ambaye amefanikiwa kukaa kwa muda mrefu kwenye Ligi ya bongo pamoja na kufanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa amewapa mbinu kali Simba ili waweze kuwaua wapinzani wao mapema kwenye hatua ya makundi.

Pluijm ambaye alifanikiwa kuifikisha Yanga hatua ya makundi ya Shirikisho, amesema anaamini Simba wananafasi kubwa ya kupata matokeo iwapo wataamua kushirikiana.

Pluijm amesema ushindani kwenye hatua ya makundi ni mkubwa hasa ukizingatia kundi ambalo wamepangwa wana nafasi ya kupenya iwapo hesabu kubwa zitakuwa ni kushinda.

"Ushindani kwenye hatua ya makundi hasa wa Ligi ya Mabingwa sio sawa na huu wa kwenye Ligi Kuu Bara, nafasi pekee ambayo itawasaidia kuweza kupata matokeo ni kucheza wakiwa ni timu na siyo kumtegemea mchezaji mmoja.

"Kundi lao lina timu nzuri hawapaswi kubeza, timu zote zimejipanga na wajue kwamba kipindi cha kwanza kwa wapinzani huwa ni za ushindani hivyo wanapaswa kuwadhidibiti mapema na kupata matokeo ya haraka," alisema Pluijm.

1 COMMENTS:

  1. Kila la kheri Simba na yes we can let's do it. Simba mechi na As Vita ni saizi yao kabisa wala Simba hawatakiwi kuingia mchecheto hata kidogo kama walivyo fanya kule Ndola Zambia kwa Nkana. Mechi hii Simba sio mechi ya kutafuta suluhu ni mechi ya kutafuta ushindi kwani mashindano haya sio ya mtoano ni mashindano ya kujikusanyia points. Na timu itakayochangamkia mapema points ndio itakayojijengea mazingira mazuri ya kusonga hatua inayofuata.Vita club ni wazuri hasa katika safu yao ya ushambuliaji lakini wanaokena wana kawikness fulani kwenye backline yao hasa inapokutana na fowadi yenye maelewano mazuri ndani ya kumi na nane ya adui. Simba wanatakiwa kucheza team work muda wote na hasa wanatakiwa kuwasisitiza washambuliaji wao kuwa makini kuzitumia nafasi wanazozitengeneza za magoli ipasavyo kufunga magoli. Kama ilivyokuwa timu nyingi lazima kunaakuwa na injini ya timu inayoiendesha timu nzima kupigania ushindi,Vita club nao wana wakali wengi wa kuisumbua Simba jumamosi ila Simba wanatakiwa kuwa makini muda wote kumchunga JEAN MAC MAKUSU MUNDELE. Huyu kijana ndio herizi ya As Vita. Ndio injini yao ya magoli,ya kuanzisha mashambulizi na ni mmaliziaji mahiri sio mchezaji kosakosa nafasi hovyo kama wachezaji wetu. Makusu Mundele yupo kwenye fomu nzuri kwani hata usipompa nafasi ya kufunga atalazimisha na ni mfungaji mahiri wa mipira ya adhabu. Ni kijana wa miaka 26 lakini alisha hangaika kiasi katika ulimwengu wa soka kwani ameshacheza Ubeligiji,Algeria, Misri na kwao Congo klabu kubwa tu kwa hivyo hana uoga hata kidogo kwenye kupambana hata ugenini sasa sikwambii akiwa kwao. Wakongo wanazadharau kiasi kwa timu za Tanzania kwa hivyo Simba wategemee physical game na mchezo wa kasi kutoka kwa As Vita kwa maana yakwamba wakongo wanaamini Watanzania wanajua mpira ila niwalaini mno na moja ya njia wanayoiaminini wakongo kutumaliza kirahisi watanzania kwenye mpira ni kutuendesha mchaka mcahaka physical game. Simba wana kocha mzuri ninaimani atakuwa mtambuzi wa mapema jinsi ya kuwakabili wakongo hao ila kama kichuya yupo fiti basi huyu ndio mti5 sahihi wa kupeleka kilio As Vita jumamosi. kwa uwezo Mungu hakuna lisilowezekana ni kujiamini na kujituma kwa malemgo bila ya hofu.
    Vile vile Simba wanatakiwa kuwa makini wakati wote hasa kwenye dakika za mwanzo za mchezo kwani ukitaka kuingia unyonge ugenini basi waruhusu wenyeji wako wajue madhaifu yako mapema lazima watakumaliza.SIMBA baada ya kushuhudia mechi ya As Vita vs El Ahly kwa nafasi ya kutosha basi nnaimani kabisa mechi ya As Vita jumamosi ni kipimo kizuri kwa wachezaji na benchi la ufundi kujua walijifunza nini na walinufaikaje katika kuwasoma wapinzani wao hao na mechi ya As Vita bila shaka ndio itakayo toa mwanga jinsi gani Simba watahimili vishindo cha El ahaly.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic